Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba Yakamilisha Usajili wa Wonlo Coulibaly kutoka ASEC Mimosas

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

KLABU ya Simba Imefanikiwa kukamilisha Usajili wa beki wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Wonlo Coulibaly baada ya mlinzi huyo kufanya vizuri katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo timu hiyo ilikwamia hatua ya nusu fainali ikifungwa na USM Alger ya Algeria.

Simba kwa sasa inasaka beki wa kati wa kusaidiana na Henock Inonga baada ya Joash Onyango kuelezwa ameomba kuondoka ili arudi Gor Mahia ya nchini Kenya alikokuwa anacheza kabla ya kusajiliwa Simba misimu miwili iliyopita. Coulibaly pia anamudu kucheza kama beki wa pembeni wa kulia na kushoto sambamba na eneo la kiungo mkabaji, hivyo kunaswa kwake kutaibeba Simba.

Yanga kumuongeza mkataba kocha Nasreddine Nabi

Kocha wa timu hiyo, Roberto Oliveira 'Robertinho' alishawapa uongozi wa Simba ni wachezaji wa aina gani anawahitaji kwenye kikosi chake msimu ujao na moja ya mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni alikiri hilo.

"Nahitaji kila nafasi iwe na ushindani, anayeingia na kutoka wafanye kazi sawa, tayari viongozi nimewapa ripoti ya nini nakihitaji naamini wanaifanyia kazi kikamilifu."

Post a Comment

0 Comments