Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa
Uongozi wa Klabu ya Simba SC Ukiongozwa na Mwenyekiti timu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’ umefanikiwa kuinasa saini ya Kiungo Mshambuliaji kutoka Niger Victorien Adebayor.
Mabosi wa timu hiyo wamekuwa wakipambana kuhakikisha wanaijenga upya timu yao kufuatia kufanya vibaya misimu miwili mfululizo kwa kushindwa kutwaa mataji.
Katika Ligi Kuu Bara wamemaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Mabingwa Young Africans wakati kwenye Kombe Shirikisho ‘ASFC’ wakiishia Nusu Fainali huku Ligi ya Mabingwa Barani Afrika wakimaliza kwenye Robo Fainali.
Usajili Mpya: Willy Eson Onana kutua Simba
Kufanya vibaya huko kumepelekea mabosi wa timu hiyo kuanza kushusha vyuma mapema ikiwa tayari wamekamilisha usajili wa mshambuliaji Onana Esomba kutoka Rayon Sport ya Rwanda kabla Jumapili (Juni 18) kukamilisha usajili wa Abebayor ambaye alikuwa nchini na timu yake ya Taifa ya Niger.
Vigogo wa Simba SC walichokifanya kuweza kufanya mazungumzo na mshambuliaji ya kukubali kujiunga na timu hiyo ni baada ya kuvamia kambi ya Niger iliyokuwa katikati ya mitaa ya Jiji la Dar ambapo ilifikia timu hiyo kabla ya kukubali kichapo cha bao 1-0 katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON’.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya timu hiyo zinaeleza kuwa Simba SC wamekubaliana kila kitu na winga huyo juu ya kujiunga na timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa kwa mkataba wa miaka miwili huku Simba SC wakilazimika kuwafuata RS Berkane ili kukamilisha usajili huo.
Tetesi za usajili Mpya: Simba SC Kusajili kimya kimya
“Viongozi walimfuata mchezaji katika hoteli ambayo amefikia na timu yake na wamefanikiwa kufanya mazungumzo, mchezaji mwenyewe amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili lakini amewaeleza namna ambayo alikosa nafasi kubwa ya kucheza kule Morocco.
“Lakini kwa sasa kilichobakia ni kwa viongozi wa Simba kwenda RS Berkane kumaliza nao ili kila jambo likae sawa na kuna uwezo wa mtu kutumwa kwenda Morocco wakati wowote.”
Yanga yafunguka ishu ya Cedric Kaze, Yannick Bangala na Tuisila Kisinda
Lakini kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Gain’, alishaweka wazi juu ya suala la kuboresha Benchi la Ufundi la timu hiyo kwa kusema kuwa wanayajua makosa waliofanya msimu huu hivyo wamejipanga kufanya maboresho makubwa katika eneo hilo ili kuweza kufanya vizuri msimu ujao.
0 Comments