Ticker

6/recent/ticker-posts

Florent Ibenge kuchukua nafasi ya Nasreddine Nabi Yanga

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Kocha wa Al Hilal ya nchini sudan Mkongomani Florent Ibenge anapewa nafasi kubwa ya kuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga baada ya kuondoka kwa Mtunisia, Nasreddine Nabi.


Mmoja wa viongozi wa Yanga amedokeza kuwa “Nabi ameondoka kwa amani kabisa, lakini tunataka kupata kocha ambaye atatuvusha kutoka hapa tulipo, kutoka pale Nabi alipotufikisha, tayari uongozi umemfikiria Ibenge na kama mazungumzo yataenda vizuri ataungana na sisi,” alisema kiongozi huyo.


Aidha, alisema wapo makocha wengine ambao klabu inafikiria kuwachukua lakini kwa sasa kipaumbele chao cha kwanza ni Mkongomani huyo.


Usajili Mpya: Willy Eson Onana kutua Simba


“Kwa sasa hao ndio makocha ambao Uongozi unaangalia uwezekano wa mmoja wapo kuja Yanga, mambo yakikaa sawa mmoja wapo atatangazwa kuwa kocha wa Yanga,” alisema kiongozi huyo.

 

Ibenge alipo hojiwa kuhusu taarifa za yeye kujiunga na Yanga alisema,bado nina mkataba na Al Hilal japo kuwa hatuchezi ligi kutokana na hali halisi ya machafuko ndani ya Sudan ambayo yameathiri ligi kuu, kuhusu Yanga siwezi kusema kitu kwa sasa kwa sababu zipo klabu nyingi zinahitaji nifanye nazo kazi.


Aidha, alisema kama kutakuwa na lolote Watanzania watajua lakini kwa sasa yeye bado ni mwajiriwa wa Al Hilal.


Nae Afisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema tangu kuandoka kwa Nabi, wamepokea CV nyingi za makocha kutoka sehemu mbalimbali.


"Tangu tulipotoa taarifa za kuachana na Nabi hadi leo hii, CV nyingi sana zimetumwa kutoka sehemu mbalimbali Afrika na nje ya Afrika, nazungumzia makocha wakubwa, uzuri ni kwamba klabu yetu kwa sasa ni kubwa na huu wingi wa makocha kutaka kufanya kazi Yanga unathibitisha kwa vitendo kazi nzuri ya viongozi kuitangaza klabu yetu, Yanga kwa sasa imeanza kuonekana kwa makocha wakubwa duniani kutamani kufanya nayo kazi," alisema Kamwe.


Alisema kwa sasa wapo kwenye mchakato unaofanywa taratibu na kwa umakini mkubwa ili kumpata kocha ambaye ataendeleza pale alipoishia Nabi.


"Kwa hiyo, niwaambie wanachama na mashabiki wanaoitakia heri Yanga, mchakato unakwenda taratibu kwa utulivu na kwa umakini mkubwa ili kutafuta kocha ambaye ataanzia  hapa ambapo tumefikia tusirudi nyuma, na mbele ninaposema ni kuendeleza utawala wetu kwenye makombe ya ndani na kumalizia kazi iliyofanywa na Nabi ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika kwa sababu yeye alifika Fainali," alisema Kamwe.


Aidha alisema wakati yanga ikiendelea na mchakato wa kumsaka mrithio wa Nabi, uongozi upo kwenye mazungumzo ya kuwaongezea mkataba makocha wasaidizi Cedric Kaze raia wa Burundi na kocha wa viungo, Mtunisia, Helmy Gueldich.


Tetesi za usajili Mpya: Simba SC Kusajili kimya kimya


Rais wa Klabu hiyo, Injinia Hersi amesema mazungumzo na walimu hao ya kutaka kuwapa mikataba mipya yanaendelea na watakachoafikiana watawaeleza wanachama na mashabiki wa timu hiyo.


Zipo taarifa kuwa Kaze anatakiwa kwa udi na uvumba na klabu za Singida Fountaine Gate na Geita Gold kwa ajili ya kuvinoa vikosi vyao.


Kaze, Gueldich na kocha wa makipa Mbrazili, Milton Nienov wote wamemaliza mikataba yao ndani ya Yanga , huku kukiwa na taarifa za Nabi kuwahitaji Kaizer Chiefs.


Post a Comment

0 Comments