Ticker

6/recent/ticker-posts

Nabi Atamba kuimaliza Marumo Gallants

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

KUELEKEA mechi ya mkondo wa pili ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika katika Uwanja wa Royal Bafokeng uliopo Rustenburg, Afrika Kusini dhidi ya Marumo Gallants Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema  mechi hiyo itakuwa ngumu, lakini akataja mbinu zake atakazotumia kutinga fainali. 

Yanga inahitaji sare yoyote ama kutokubali kufungwa zaidi ya bao moja ili kutinga fainali ya michuano hiyo na kuandika rekodi ya klabu, tangu kuanzishwa kwake miaka 88 iliyopita.

Hiyo ni kutokana na kushinda nusu fainali ya kwanza Jumatano iliyopita kwa mabao 2-0 katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Robertinho amaliza kazi Simba Afyeka na kutaja majembe anayotaka

Akihojiwa jana, Nabi alisema kwa sasa anaendelea kuwaongezea wachezaji wake umakini na kutumia vema nafasi wanazotengeneza ili kutafuta bao la mapema katika ardhi ya Afrika Kusini jambo litakalowachanganya Marumo Gallants.

Alisema anajua ubora wa wapinzani wao wanapokuwa nyumbani na wanahitaji kutumia madhaifu yao hasa katika safu yao ya ushambuliaji kutafuta bao la mapema katika kipindi cha kwanza.

Alisema ameona madhaifu ya mpinzani wao huyo hasa katika safu ya ulinzi, lakini akiwataka mabeki wake kuwa makini kutokana na uwezo wa safu ya ushambuliaji ya Marumo katika kutengeneza nafasi.

“Marumo Gallants si timu mbaya kwa sababu washambuliaji wake ni wazuri, mechi ya kwanza waliweza kutusumbua, lakini safu yao ya ulinzi inashida, tukiweza kutumia madhaifu yao tutarejea nyumbani tukiwa tunacheza fainali, lakini tusipokuwa makini tutaweza kupoteza hii mechi,” alisema Nabi.

Aidha, kocha huyo alisema kukosekana kwa nyota wake, Bernard Morrison, kwenye mchezo huo hakutaathiri kitu chochote kwa sababu ya kuwa na kikosi kipana hususan mbadala.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema wamefika salama na wachezaji wote wapo salama na tayari kwa mchezo huo. “Tumefika salama, timu imefanya mazoezi katika uwanja uliopo katika hoteli tuliyofika, kazi iliyopo sasa ni wachezaji kufuata yale wanayoelekezwa na kocha ili kuhakikisha tunafanikiwa kucheza fainali ya Afrika,” alisema Kamwe.

Post a Comment

0 Comments