Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga Yatuma Ujumbe Mzito Simba Kuhusu Ubingwa Wa Ligi

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

UONGOZI wa Yanga, umeweka wazi kuwa, wapinzani wao ndani ya Ligi Kuu Bara hawataamini namna watakavyofanikiwa kutetea taji hilo msimu huu kutokana na mipango waliyonayo.

Timu hiyo kwa sasa inaongoza ligi ikiwa na pointi 62 baada ya kucheza mechi 23, inafuatiwa na watani zao wa jadi, Simba walio nafasi ya pili na pointi 54.

Ofisa Habari wa Yanga Ally Kamwe, amesema kuwa, wapo ambao wanafikiria timu hiyo itapata matokeo mabaya kwenye mechi zijazo, huku yeye akibainisha kwamba haitakuwa hivyo.

“Tumeanza kuhesabu mechi ambazo tunashinda kwa sasa na malengo yetu ni kutofungwa mpaka pale ambapo tutakamilisha ligi na kuanza kwa mara nyingine tena msimu mpya.

“Wale ambao wanafikiria kwamba tutapoteza hawataamini kwa sababu hatuna mpango wa kupoteza na malengo yapo kwenye kushinda mechi zetu.

“Mashabiki wazidi kujitokeza kwenye mechi ambazo tunacheza, tunahitaji kufanya kazi kubwa na tunaamini kila kitu kitakuwa sawa,” alisema Kamwe.

Yanga katika mechi saba ilizosalia nazo, inatakiwa kushinda nne mfululizo zijazo ili kujihakikishia kutetea ubingwa wa ligi hiyo ambao wana rekodi ya kuubeba mara nyingi zaidi ambazo ni 28.


Post a Comment

0 Comments