Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga yatangaza vita kwa US Monastir

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Uongozi wa Yanga umeweka wazi kuwa maandalizi kuelekea mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Monastir ya Tunisia yanaendelea vizuri.

Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa ugenini nchini Tunisia Yanga ilipoteza kwa kushuhudia ubao ukisoma US Monastir 2-0 Yanga watakuwa na kazi ya kusaka ushindi Jumapili.

Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe amesema waache Waarabu hao wa Tunisia waje Uwanja wa Mkapa wamalizane nao kwa kuwa wana deni nao.

”Maandalizi ya mchezo wa Jumapili yanaendelea vizuri na uongozi umeanza maandalizi ya kishindo kuelekea mchezo huu.

“Ni mbinu nyingi ambazo zipo na benchi la ufundi mliona pale Chamazi baada ya wale Geita kutaka kutujaribu hawakuamini walichokiona hivyo mashabiki na wanachama mjitokeze kwa wingi na tumefungua kampeni rasmi kwa ajili ya mchezo wetu wa kimataifa,” amesema.

Tayari tiketi zimeanza kuuzwa kwa mashabiki na wanachama wote Tanzania.

Slogan kwajili ya mchezo huo wa kimataifa Yanga Inasema:’Full House, Full Shangwe......Waje Tumalizane.

Nabi haturudii tena makosa dhidi ya US Monastir

Post a Comment

0 Comments