Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba, Yanga zamuwinda Cheickna Diakite

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

KLABU ya Yanga imeanza rasmi mazungumzo na winga wa Real Bamako ya Mali, Cheickna Diakite lakini staa huyo ameweka wazi kuwa kuna wakala wa Simba amemcheki wakala wake. 

Juzi Diakite alicheza dakika 45 za kipindi cha pili dhidi ya Yanga, kocha Nasreddine Nabi akateta naye mara baada ya Mchezo huo.

Baada ya mchezo huo wa Kundi D wa Kombe la Shirikisho Afrika, Real Bamako ikipoteza kwa mabao 2-0 mchezaji huyo alifunguka alichozungumza na kocha huyo.

Diakite amethibitisha kuwa, Yanga inataka huduma yake ambapo hata baada ya kuongea na Nabi ilikuwa ni kumpongeza kwa kiwango chake, pia akimkaribisha kuja kujiunga na klabu hiyo.

Diakite alisema tayari mabosi wa Yanga walimfuata mara baada ya timu hizo kukutana jijini Bamako na pambano baina yao kumalizika kwa sare ya 1-1, ambapo walipeana nafasi ya kuendelea kuzungumza, huku akiitaja Simba pia kumsaka kupitia wakala mmoja wa wachezaji.

“Yanga ndio wamenifuata na kuongea nami, niliongea nao kule nyumbani baada ya mchezo wa kwanza, lakini hata hapa nimeongea na kocha wao (Nabi), ameniambia anapenda kiwango changu nami ni kijana natakiwa kuwa na njaa ya mafanikio kwa kujituma zaidi, amenikaribisha kama nitahitaji changamoto mpya nijiunge nao,” alisema Diakite na kuongeza;

“Yanga ni timu nzuri naona jinsi watu wa hapa walivyo na hamasa, kuna kaka zangu hapa Djigui (Diara) na Mamadou (Doumbia), lakini wakala mmoja pia ameniambia kuna timu inaitwa Simba inanihitaji. ”Aidha Diakite amefichua, licha ya kutakiwa na vigogo hao wa Kariakoo klabu yake inapiga hesabu za kumuuza nchini Ufaransa mwisho wa msimu huu ingawa bado dili hilo halijafika mwisho.

“Ilikuwa niondoke muda mrefu lakini waliniambia nisubiri kwanza tumalize msimu huu hasa hizi mechi za CAF, kuna timu ya Ufaransa inazungumza na uongozi wa klabu unajua bado nina mkataba kwahiyo wao pia wataamua ingawa hayo mazungumzo hayakufikia mwisho, nitajua baada ya msimu kumalizika wapi nitakwenda.”

Kocha Nabi anapiga hesabu ya kunasa winga teleza ili kuimarisha kikosi hicho licha ya sasa kuwa na mawinga kama Tuisila Kisinda, Jesus Moloko, Yanga ina mawinga wengine kama Bernard Morrison, Farid Mussa na Dickson Ambundo ambao hawajampa kile anachokitaka. 

Yanga hesabu zao ni kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya CAF msimu huu na endapo wataifunga Monastir Jijini Dar es Salaam itafuzu robo fainali kwa kishindo.

Yanga yamuwinda Cheickan Diakite wa AS Real Bamako

Post a Comment

0 Comments