Ticker

6/recent/ticker-posts

Nabi: Sina Tatizo Na Feisal Salum ‘fei Toto’ Nipo Tayari Kumpokea

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema kuwa hana tatizo na kiungo wake mshambuliaji Feisal Salum ‘Fei Toto’ na yupo tayari kumpokea kama atakuwa tayari kurejea kikosini hapo.

Nabi ameyasema hayo ikiwa ni siu chache tangu kiungo huyo apeleke barua ya kusitisha mkataba wa kuitumikia Yanga katika Makao Mkuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Kiungo huyo amefikia hatua ya kuwasilisha barua hiyo TFF akitaka kusitisha mkataba wake, baada ya Kamati ya Hadhi na Sheria za Wachezaji ya TFF kusema ni mchezaji halali wa Yanga, huku klabu yake ikimtaka kurudi kambini haraka.

Nabi alisema Fei Toto bado kijana wake, hivyo hana tatizo na yeye, huku akimshauri kurejea kambini kuipambania timu iliyo hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Aliongeza kuwa, hakuna asiyefahamu ubora na kiwango cha Fei Toto, hivyo kama akirejea atamkaribisha kwa mikono miwili kuendelea kuichezea Yanga.

“Kama ningepewa nafasi ya kumshauri Fei Toto, basi ningemwambia arudi Yanga, na mimi kama kocha nitampokea kwa mikono miwili.

“Lakini kama yeye mwenyewe hataki, basi namtakia kila la heri, ingawa nafahamu bado ni mchezaji halali wa Yanga mwenye mkataba. Kwangu bado ana nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi changu kutokana na kiwango alichonacho,” alisema Nabi.

Yanga Yamtaka Feisal Salum Kuripoti Kambini Haraka

Post a Comment

0 Comments