Ticker

6/recent/ticker-posts

Mo Dewji: Kuna Watu Ndani Ya Simba Wananikwamisha ipo siku antawataja hadharani

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Mwekezaji na Rais wa Heshima wa Klabu ya Simba Mohamed Dewji ‘Mo’ amesema kuna watu ndani ya klabu hiyo wanamkwamisha kwenye mambo mbalimbali na kuongeza kuwa kama wakiendelea ipo siku atawataja majina yao hadharani.

Mo amefunguka mambo mengi ambayo ulikuwa huyajui alipofanya mahojiano ‘exclusive’ Mwandishi mahiri wa habari za michezo, salehjembe.

“Kuna tatizo, Kuna makosa ambayo yamefanyika kwenye usajili, tumesajili wachezaji ambao hawa-perform kwa hivyo mara Hii tunakuja na mfumo mpya, tunabadilisha system nzima ya scouting, tutakuwa na watu wa ndani watashirikiana na watu wa nje ambayo ni professional,” Rais wa Heshima wa Simba, Mohammed Dewji.

Kuelekea mchezo wa leo wa Taifa stars dhidi ya Uganda, Mohammed Dewji amenunua tiketi 5,000 kwa ajili mashabiki katika mchezo wa kuwania kufuzu AFCON kati ya Tanzania na Uganda utakaopigwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa majira ya saa 2:00 usiku.

Wengine ni Azim Dewji amenunua tiketi 1,000, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah  na Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mangungu kwa pamoja wamenunua tiketi 1,100.

Habari Kubwa Za Magazeti Ya Leo March 28, 2023

Post a Comment

0 Comments