Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohamed Dewji Maarufu kama 'Mo', amemteua kwa mara nyingine Salim Abdallah ‘Try Again’, kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba.
Mo amefanya uteuzi huo katika hafla fupi ya kuwaaga wajumbe waliomaliza muda wao akiwamo Kassim Dewji, Mwina Kaduguda na Hussein Kita.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mohamed Dewji, alisema kuwa anaimani na Try Again' ndio maana amempa nafasi nyingine na anaamini ataendelea kuiongoza Simba kufikia mafanikio makubwa barani Afrika.
"Umefanya kazi nzuri ninaimani na wewe, nategemea utaifikisha Simba kwenye mafanikio makubwa ya soka barani Afrika na duniani kwa ujumla, " alisema Mo.
Kwa upande wa Try Again, alisema anafurahi kuwa sehemu ya uongozi katika bodi hiyo na kwamba atahakikisha anaendelea kuitendea haki nafasi aliyopewa kwa mara nyingine kuifanya Simba kuwa imara.
“Asante sana ndugu Mohamed Dewji kwa imani yako juu yangu, nakuahidi utendaji bora kwenye nafasi hii ili kwa pamoja tunaweza kuifikisha Simba kwenye mafanikio makubwa ambayo inastahili,” alisema Try Again.
Uongozi Yanga Waipongeza Simba
Mo alitumia hafla hiyo kuwapa vyeti wajumbe watatu ambao ni Murtaza Mangungu, Haroub Seleman na Asha Baraka ambao bado wako katika bodi hiyo wakipita kwa upande wa wanachama baada ya kuchaguliwa hivi karibuni.
Mo alimteua Try Again kuchukua nafasi yake Septemba mwaka 2021, baada ya kubanwa na shughuli zake za biashara ambapo amefanya kazi nzuri kabla ya kumteua tena kuongoza bodi hiyo.
Wakati huo kikosi cha Simba kimeingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa hatua ya 16-bora ya Kombe la Shirikisho la Azam (FA Cup) dhidi ya African Sports kutoka Tanga.
0 Comments