Ticker

6/recent/ticker-posts

Mayele, Mzize Wagawana Ufalme ndani ya Yanga Mashabiki Watamba

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Mashabiki wa Yanga kwa sasa wanatamba kwa kuwa safu yao ya ushambuliaji inafunga mabao, Jambo hilo ni furaha pia kwa benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, kutokana na wingi wa michezo na mashindano wanayoshiriki.

Yanga wanashiriki Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho la Azam Sports na Kombe la Shirikisho Afrika, jambo ambalo linahitaji mapumziko kwa wachezaji kwa kuwa michezo huwa ni mingi inafuatana mfululizo.

Mayele ndiye kinara wa upachikaji mabao katika ligi kuu huku Mzize akiwa kinara wa upachikaji mabao katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Mayele, Mzize Wagawana Ufalme Yanga

Jambo linalowapa jeuri Mashabiki na Wanachama wa Yanga ni kutokana na washambuliaji wao wawili, Fiston Mayele na Clement Mzize kugawana ufalme katika kupachika mabao ndani ya timu hiyo.

Mayele ndiye kinara wa upachikaji mabao katika ligi kuu akiwa anaongoza kwa kufunga mabao 15.

Katika kuonesha kuwa washambuliaji hao wamegawana ufalme wa kupachika mabao, Mayele akiwa ni kinara kwa upande wa ligi kuu, Clement Mzize naye amejiwekea ufalme wake.

Nabi Ategua Mitego Ya Real Bamako

Mshambuliaji huyo ndiye kinara wa upachikaji mabao katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports baada ya kufanikiwa kufunga mabao sita.

Mzize ana nafasi zaidi ya kufunga mabao baada ya Yanga kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, huku Mayele naye akiwa na matumaini ya kuongeza mengine katika mechi saba za Ligi Kuu Bara zilizosalia.

Post a Comment

0 Comments