Ticker

6/recent/ticker-posts

Clement mzize Azidi Kumkosha Nabi

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

KOCHA Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema anakoshwa na kiwango kinachoonyeshwa na straika mzawa Clement mzize kwa dakika chache anazompa.

Mzize ambaye amepandishwa kutoka kikosi B amekuwa akizitumia vizuri dakika chache anazopewa na kocha Nabi na hivyo kumuweka kwenye wakati mgumu straika Chrispin Ngushi kupata nafasi ya kucheza.

Katika mabao matatu aliyofunga Ligi Kuu Bara, Mzize ameisaidia Yanga kupata pointi sita baada ya kufunga dhidi ya Kagera Sugar ilikuwa 1-0 na  KMC timu yake ikishinda 1-0 pia alifunga mojawapo kati ya mabao 3-0 dhidi ya Polisi Tanzania.

Jambo ambalo kocha Nabi alisema  bado ni kijana mdogo ndio maana wanampa dakika chache ili kumjengea kujiamini kufanya makubwa zaidi kwenye karia yake, akiamini kuna kitu anakiongeza kila anapocheza.

"Kadri ninavyompa dakika za kucheza ndivyo kiwango chake kinazidi kukua siku hadi siku, kikubwa akijengeka kujiamini atafanya mambo makubwa zaidi kwani soka linahitaji ushindani, nidhamu na kujituma kwa bidii;

Aliongeza "Pia maarifa yake ya kazi yatazidi kuongezeaka maana atajifunza mbele ya wengine ili kuboresha kiwango chake.

Simba, Yanga zamuwinda Cheickna Diakite

Ukiachana na mabao ya Ligi Kuu, Mzize anamiliki mabao sita kwenye Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), tofauti na ngushi ambaye kwa msimu huu hana bao hata moja, hivyo atahitaji kupambana zaidi ili kumshawishi kocha kumpa dakika za kucheza.

Baada ya Mzize kuonyesha kiwango ligi ya ndani, juzi kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Bamako ya Mali, Nabi alimpa dakika 15.

Dakika ya 75 Nabi alifanya mabadiliko kwenye mchezo huo alimtoa  Kennedy Musonda, akaingia Mzize ambaye aliongeza presha kwa mabeki wa Bamako.

Hilo pia Nabi alilizungumzia kwamba "Muda niliompa ni sahihi, kuna kitu atakuwa amekipata kwenye michuano hiyo inayohitaji kutumia nafasi kwa umakini zaidi."

Post a Comment

0 Comments