Ticker

6/recent/ticker-posts

Bilionea Yanga Atoa Kauli Ya Kutisha Akielekea Congo

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 


BILIONEA wa Yanga, Ghalib Said Mohammed ‘GSM’ jana Alhamisi kwa mara ya kwanza alisafiri na kikosi cha timu kwenye safari ya mashindano rasmi na kutoa tamko zito kuwa Yanga wanautaka ubingwa wa mashindano hayo.


Yanga ndio wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo kwenye mashindano hayo mpaka sasa wanaongoza msimamo wa kundi D baada ya kufanikiwa kukusanya pointi 10 katika michezo yao mitano ya kwanza.


GSM pamoja na baadhi ya viongozi wa juu wa Yanga akiwemo rais wao Injinia Hersi Said na Makamu wa Rais, Arafati Haj jana Alhamisi waliongozana na sehemu ya kikosi cha wachezaji wa Yanga ambao hawakuwa na majukumu ya timu za Taifa kuelekea nchini DR Congo kwa ajili ya mchezo wao wa mwisho wa kukamilisha ratiba ya hatua ya makundi watakapovaana na TP Mazembe, utakaopigwa Aprili 2, mwaka huu.


Akizungumza muda mfupi baada ya kujiunga na kikosi kwenye safari hiyo GSM alisema: “Tunashukuru kwa kuwa kikosi chetu kimefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya mashindano haya lakini tunajua mchezo wetu dhidi ya TP Mazembe utakuwa mgumu na muhimu.


“Tunataka kushinda mchezo huu lakini kwa nafasi ya pekee tuna malengo ya kushinda ubingwa wa mashindano haya, tunajua sio rahisi lakini tupo tayari kupambana kufanikisha hilo na tunaamini katika ubora wa kikosi chetu.”


Habari Kubwa Za Magazeti Ya Leo March 31, 2023


Post a Comment

0 Comments