Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga yatabiriwa makubwa Kombe la Shirikisho Barani Afrika 2023

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Mwandishi wa Habari za Michezo Gift Macha amesema, Kikosi cha Yanga kimeimarika kwa kiasi kikubwa, baada ya kuambulia alama moja kwenye Mchezo wa Mzunguuko watatu, Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Jana (Februari 26) Yanga ilicheza ugenini mjini Bamako-Mali dhidi ya AS Real Bamako katika Uwanja wa Machi 26, na kuambulia sare ya 1-1.

Gift Macha ambaye pia ni Mchambuzi wa vipindi vya Michezo Azam TV (Azam Media), amesema kikosi cha Yanga kimekua na muonekano tofauti na ilivyokuwa msimu ulipopita, hivyo anaamini kinaweza kufanya makubwa na maajabu kwenye Michuano ya Kimataifa msimu huu.

Amesema katika mchezo wa Jana, Yanga ilicheza bila kuogopa ugenini, na kikosi chake kilikuwa chepesi kukaba kilipopoteza mpira, huku kikimiliki vizuri dhidi ya wapinzani wao.

“Yanga wameimarika sana kama timu. Wanamiliki mpira vizuri.Wakipoteza wanakaba kwa haraka sana. Wana kasi katika kushambulia na pia wana wachezaji mahiri wa kuamua mechi. Nazidi kuwaona mbali.” amesema Gift Macha

Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi kutoka nchini Botswana Joshua Bando, Yanga ilitangulia kupata bao kupitia kwa Mshambuliaji Fiston Kalala Mayele dakika ya 60 ya mchezo kabla ya Kone hajafunga bao la kusawazisha dakika ya 90.

Ratiba ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika inatarajiwa kuendelea siku ya Jumatano (Machi 08) ambapo Yanga itawakaribisha AS Real Bamako katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Post a Comment

0 Comments