Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga Yakaribia Ubingwa Ligi Kuu Tanzania Bara

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

USHINDI wa bao 1-0 iliyo upata Yanga dhidi ya KMC umewafanya mabingwa hao watetezi kuzidi kuukaribia tena ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa pili mfululizo.

Katika Mchezo huo Mshambuliaji chipukizi wa Yanga, Clement Mzize, alifunga bao pekee lililo ipatia timu yake ushindi katika mechi ya raundi ya 24 ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KMC FC iliyochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Yanga sasa imefikisha pointi 62, ikiwaacha watani zao wa jadi, Simba ambao juzi walivutwa shati na Azam FC kwa tofauti ya pointi nane huku KMC ambao walikuwa wenyeji wa mechi hiyo wamesalia na pointi zao 23.

Mzize aliwanyanyua mashabiki wa Yanga waliokuwa uwanjani hapo baada ya kuukwamisha mpira wavuni dakika ya 38 kutokana na uzembe wa kipa wa KMC, David Kissu.

Bao hilo lilitokana na kona ya Tuisila Kisinda ambayo haikuonekana ya hatari sana, lakini kipa huyo akiruka juu kutaka kuupangua pembeni kwa mkono wa kushoto, badala yake akaurudisha ndani kwenye kundi la wachezaji wa timu zote mbili na Mzize kama vile aliyeokota dodo chini ya nguzo ya umeme, akaupiga kwa mguu wa kulia na kuujaza wavuni.

KMC ndiyo ilianza kufika langoni mwa Yanga dakika za mwanzo tu mwa mchezo, wakati, Emmanuel Mvuyekule, alipopiga shuti akiwa nje ya eneo la hatari, lakini mlinda mlango wa Yanga, Djigui Diarra, alilitema na kukosa muunganishaji wa kumalizia mpira huo.

Yanga ilijibu muda huo huo kwa shuti na Salum Abuobakar 'Sure Boy' ambalo Kissu alilipangua lakini lilionekana kumshinda nguvu na kuelekea wavuni, lakini ukatoka sentimeta chache langoni mwake.

Kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko ambayo yalionekana kuichangamsha mechi hiyo, lakini kosa kosa iliendelea kutawala katika mechi hiyo hasa kwa upande wa vinara hao wa ligi.

Mzize angeweza kupiga 'hat-trick' katika  mchezo wa jana, baada ya kukosa mabao mawili ya wazi, moja likiwa kwenye dakika ya 61 ambapo alimzidi mbio, Abrahim Ame na kubaki na Kissu, lakini aliokenana kujifikiria mno, kabla ya beki huyo kumkuta na kuufagia mpira huo, wakati benchi la ufundi likiwa limesimama tayari kushangilia bao.

Katika mchezo huo Kinara wa mabao wa Ligi Kuu, Fiston Mayele aliyeingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Mzize angeweza kupachika bao la pili na kufikisha mabao 16 kibindoni mwake kama kombora alilopiga karibu na lango la KMC kutokana na krosi ya Joyce Lomanisa lisingegonga nguzo ya juu na kurejea uwanjani dakika sita kabla ya mechi kumalizika.

Nabi ataka Mudathir awe kama Feisal Salum 'Fei Toto'


Post a Comment

0 Comments