Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba Yaanza Kwa Kichapo Ligi Ya Mabingwa Afrika

 

KLABU ya Simba Imeanza kwa kichapo  katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya baada ya kufungwa bao 1-0 katika Uwanja wa Jenerali Lansana Conte nchini Guinea.


Wenyeji Horoya walipata bao dakika ya 18 kupitia kwa Pape Ndiaye kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Mohamed Wonkoye.


Mlinda mlango Aishi Manula alicheza mkwaju wa penati dakika ya 72 uliopigwa na Ndiaye baada ya mlinzi Joash Onyango kuunawa mpira ndani ya 18.


Dakika ya 79 nahodha John Bocco almanusura aipatie Simba bao la kusawazisha kufuatia mpira wake kutoka nje kidogo ya lango la Horoya baada ya kupokea pasi ya Kibu Denis.


Mchezo unaofuata utakuwa Februari 18 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco.


Kikosi cha Horoya

Camara, Coullibaly, Samassekou, Samake, Diaw, Kante (Naby 77), Camara, Wonkoye (Sebe 62′) Soumah (Coumbassa 86′), Ndiaye (Amamou 77′) Camara ( Ismael Camara 77′).


Walioonyeshwa kadi: Coullibaly 65′ Fode Camara 90.


Kikosi cha Simba

Manula, Kapombe Zimbwe Jr, Onyango, Henock, Kanoute, Sakho (Bocco 45′), Sawadogo (Phiri 61′), Baleke (Kibu 61), Mzamiru, Chama.


Walioonyeshwa kadi: Zimbwe Jr 60′, Kanoute 64′ Onyango 70′ Bocco 73′


Post a Comment

0 Comments