Ticker

6/recent/ticker-posts

Sakho Tutapambana na Kuhakikisha Tunashinda

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Pape Sakho ameweka wazi kuwa lengo ni kuhakikisha wanashinda ugenini dhidi ya Horoya katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigiwa Jumamosi.


Sakho amesema kila mchezaji anajua umuhimu wa mchezo huo na yupo tayari kuhakikisha anapigania timu kupata matokeo mazuri ugenini.


Kuhusu kukosekana kwa kiungo mshambuliaji, Saido Ntibazonkiza, Sakho amesema natamani angekuwepo kikosini kutokana na ubora na uzoefu wake lakini siku zote majeruhi sio kitu kizuri kwa mchezaji.


“Maandalizi yetu ni mazuri, malengo yetu ni kushinda ugenini tutapambana ili kufanikisha hilo.


“Tunajua haitakuwa mechi rahisi, tutakuwa ugenini lakini tupo tayari kwa mpambano na mashabiki wetu tunawaomba mtuombee ili tukatimize malengo,” amesema Sakho.


Post a Comment

0 Comments