Ticker

6/recent/ticker-posts

Nabi: Yanga tuna njaa ya mafanikio

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema timu yake itashuka dimbani kucheza mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa na njaa ya mafanikio.

Yanga inatarajia kuikaribisha TP Mazembe katika mechi ya Kundi D itakayochezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. 


Nabi alisema wamejiandaa kisaikolojia kuhakikisha wanapata matokeo chanya ili kufikia malengo ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).


Kocha huyo alisema wanafahamu mechi hiyo haitakuwa nyepesi kwa pande zote mbili lakini wana matumaini watatumia vizuri uwanja wa nyumbani.


“Sioni kama tunastahili kufanya makosa kama yale tuliofanya Tunisia, tunajua mechi haitakuwa rahisi, tunakwenda kukutana na timu nyingine bora lakini tunapaswa kucheza kama Yanga yenye njaa ya mafanikio, wao wametoka kushinda mchezo wa kwanza, hivyo ari yao itakuwa juu,” alisema Nabi.


Kocha huyo aliongeza amewaangalia vizuri  TP Mazembe katika mechi zake mbalimbali na kuona ubora pamoja na  madhaifu yao, hivyo atahakikisha anafanyia kazi ili kufanikisha malengo ya timu yake.


Aliongeza hawatarajii kurudia makosa waliyofanya katika mchezo wa kwanza uliochezwa ugenini Tunis ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi mipira ya Set Pieces ambayo walifungwa na US Monastir.


Wakati huo huo Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, amesema suala la kiungo wao Feisal Salum ‘Fei Toto' liko vizuri na keshokutwa atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaokuwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.


“Fei Toto ni mchezaji halali wa Yanga, suala la yuko kambini au hayupo, Jumapili tutakapocheza dhidi ya TP Mazembe, atakuwa sehemu ya wachezaji wote uwanjani,” alisema Kamwe na kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mechi hiyo.


Inadaiwa Fei Toto amelipwa Sh. milioni 350 ili kusaini mkataba Mpya wa miaka miwili na sasa atapokea mshahara wa Sh. milioni 15 kwa mwezi.


‘Robertinho’ Awaondoa Hofu Mashabiki Wa Simba Asema Ushindi Lazima

Post a Comment

0 Comments