Yanga itakuwa ugenini kuwakabili AS Real Bamako mjini Bamako-Mali Jumapili (Februari 26) katika Uwanja wa Machi 26, chini ya usimamizi wa Mwamuzi kutoka nchini Botswana Joshua Bondo.
Kocha Nabi amesema amekua na zaidi ya mfumo mmoja anaoutumia dhidi ya timu pinzani katika Michezo ya Ligi Kuu na ile ya Kimataifa, hali ambayo inamuaminisha kuwa na uhakika wa kupambana popote Barani Afrika.
Yanga Yakaribia Ubingwa Ligi Kuu Tanzania Bara
“Kitu bora tumetanua matumizi ya mifumo yetu na tunaweza kubadilika kulingana na mpinzani ambaye tutacheza naye kwa ubora wake, hii ni faida yetu kubwa,”
“Nimewaambia wachezaji, kuwa kitu ambacho kitatupa thamani kubwa ni kwenda kuendeleza ushindi wetu, ingawa nafahamu haitakuwa rahisi, tunapaswa kujitoa kwa kucheza kwa umakini mkubwa.” amesema Kocha Nabi
Ushindi dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo umeiweka Yanga pazuri katika msimamo wa Kundi D, ikishika nafasi ya nne kwa kuwa na alama tatu, ikitanguliwa na US Monastir ya Tunisia yenye alama nne.
TP Mazembe inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama tatu, huku AS Real Bamako ikiburuza Mkia kwa kuwa na alama moja.
0 Comments