Ticker

6/recent/ticker-posts

Nabi ataka Mudathir awe kama Feisal Salum 'Fei Toto'

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kocha Mkuu wa Yanga Nassredine Nabi amesema kuwa anataka kumtengeneza Mudathir kuwa bora kama ilivyokuwa kwa kiungo wa timu hiyo ambaye yupo nje kwa sasa Feisal Salum 'Fei Toto' kwa kuwa anamuona kuwa ana kitu anaweza kuongeza kwenye kikosi chake.

Mudathir alionyesha kiwango cha juu kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika wikiendi iliyopita dhidi ya TP Mazembe na kufanikiwa kufunga bao moja kwenye ushindi wa mabao 3-1, alicheza nafasi ya kiungo mchezeshaji namba (10) kwa mara ya kwanza tangu amejiunga na timu hiyo kwenye dirisha dogo la usajili.

Mudathir ambaye aliwahi kuwika akiwa na Azam FC alisema ni kweli amecheza nafasi hiyo kwa mara ya kwanza lakini hakukurupushwa aliandaliwa mapema na kocha na wachezaji wenzake pia walikuwa na taarifa ya yeye kucheza nafasi hiyo ambayo mara nyingi alikuwa akicheza Fei Toto.

"Nafurahi kupata meseji nyingi kutoka kwa wadau wa soka kuwa nimecheza kwa ubora kwenye nafasi hiyo, pia kocha aliniambia nimefanya kile alichokuwa anataka nikifanye, hili limenipa nguvu lakini naomba kukiri kuwa ubora ulitokana na wachezaji wote kuwa imara.

"Timu yote kwa ujumla ilicheza kwa vizuri bila kuangalia mchezaji mmoja mmoja hili ni moja ya kitu muhimu kikosini, pia kila mchezaji anaweza kucheza nafasi nyingi uwanjani akiandaliwa na akikubali kufanya majukumu."

Mastaa Yanga wapewa Sh130 milioni baada ya kuifunga TP Mazembe

Mudathir alisema ilikuwa ngumu kwake pamoja na kucheza vizuri na kupata nafasi ya kufunga kuna muda alikuwa anasahau majukumu yake na kurudi nyuma kukaba kitu ambacho wachezaji wenzake walikuwa wanakiona na kumkumbusha.

"Nimezoea kukaba kucheza namba sita, nilipopewa nafasi ya juu kuna muda nilikuwa nasahau majukumu nashuka chini lakini wachezaji wenzangu uwanjani wananishtua na kunitaka nirudi juu na ndio maana nakiri kuwa ubora wa timu nzima ndio umenifanya kuonekana bora.


"Nipo tayari kucheza nafasi yoyote kikubwa ni kuipambania timu na kama kocha kaona kitu kwangu akaamua kunipa nafasi siwezi kukataa kufanya kwasababu kazi yangu ni kucheza, naamini baada ya muda nitakuwa bora zaidi."

"Mudathir ni mchezaji mzuri lakini hana maamuzi ya haraka akiwa kwenye maeneo mazuri kama ilivyo kwa Fei Toto, naamini kadri muda unavyozidi kwenda ataweza kuingia kwenye mfumo na kuwa bora kama alivyo kuwa kwa Fei Toto, hii ni kazi yangu na naamini kuwa nitajitahidi kuifanya kwa ufasaha.

"Nataka kuona zile kazi alizokuwa anazifanya Fei ambaye tulimtegeneza kuwa bora basi Mudathir anazifanya, kwangu bado naamini kuwa Fei ni mchezaji mkubwa sana hapa nchini, lakini hata Mudathir baadaye atakuwa kwenye kiwango kizuri zaidi."

Nabi alisema kiungo huyo ni mwepesi wa kufanyia kazi mambo anayo elekezwa hivyo anaamini ataweza kuisaidia timu na kuwa bora na atafunga sana kama atakuwa mwepesi wa kufanya maamuzi kwenye maeneo sahihi.

Simba Sc Wakanusha Kumtimuwa Robertinho

Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amepongeza mastaa wenzake kwa umoja waliouonyesha kuhakikisha wanaipambania timu na kuipa matokeo bora ili kuhakikisha wanafikia lengo.

"Mchezo ulikuwa mzuri na wa ushindani umoja na ubora wa wachezaji ndio uliamua matokeo bado tuna nafasi nzuri ya kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi nyingine ili kuendeleza furaha kwa mashabiki na kufikia malengo."

Post a Comment

0 Comments