Ticker

6/recent/ticker-posts

Manchester United Kumsajili Harry Kane wa Tottenham Hotspur

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Manchester United bado wana nia ya dhati ya kumsajili Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Harry Kane  katika dirisha la usajili majira ya joto ili kuboresha safu yao ya Ushambuliaji.

Kwa mujibu wa Jarida la Football Insider, Tottenham Hotspurs tayari wameanzisha mazungumzo na nahodha wao kuhusu kandarasi mpya.

United wanafuatilia kwa karibu ,huku mkataba wa sasa wa nyota huyo wa Uingereza na Klabu yake ya Tottenham Hotspurs unatarajiwa kutamatika 2024, ikimaanisha kwamba, ikiwa hataondoka msimu huu wa majara ya joto,basi Kane ataondoka bure.

United inataka kusajili mshambuliaji mpya kabla ya kuanza kwa msimu ujao baada ya kumsajili Wout Weghorst kama mshambuliaji wa dharura katika dirisha la mwezi Januari.

Anthony Martial ndiye mshambulizi pekee tegemeo baada ya marcus rashford katika klabu hiyo lakini amekuwa akiandamwa na majeraha msimu huu.

United ikimpata Kane itakuwa imeboresha safu ya Ushambuliaji kwa kiasi kikubwa na anaweza kufanya takriban timu yote kuwa bora zaidi kutokana na uwezo wake wa kucheza.

Tottenham wakiwa katika hatua za awali za mazungumzo na Kane, Bayern Munich wameonyesha kuvutiwa na Mshambuliaji huyo raia wa Uingereza hivyo kuiweka Tottenham katika wakati magumu kumshawishi kane kusalia klabuni hapo miezi ijayo.

United wana matumaini kwamba watakuwa mstari wa mbele kumsajili Kane, hata hivyo, kukiwa na uwezekano wa kuhamia nje ya nchi kutokana na hamu ya nahodha huyo wa Uingereza kuboresha rekodi ya Alan Shearer ya mabao 260 ya Ligi Kuu ya Uingereza. Hivi majuzi alikua mfungaji bora wa muda wote wa Tottenham, akishinda jumla ya mabao 266 ya Jimmy Greaves katika mashindano yote.

Kama United watashindwa katika majaribio yao ya kumsajili Harry Kane,basi wanaweza kuelekeza nguvu zao kwa Mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen anaye ichezea Napoli ya Italia.

Robertinho Afichua Siri Ya Ushindi Dhidi Ya Vipers Sc


Post a Comment

0 Comments