Ticker

6/recent/ticker-posts

Kocha Simba Aahidi kuibuka na Ushidi dhidi ya Horoya

 

KOCHA Mkuu wa Simba Mbrazil, Roberto Aliveira amesema kuwa kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa afrika dhidi ya Horoya wamejipanga kuibuka na Ushindi, huku winga Pape Sakho akisema wanachoangalia si mechi hiyo tu, bali ni kuvuka kwenye hatua hiyo ya makundi.


"Tunakwenda kucheza mechi ya mashindano ya kimataifa, ni muhimu kwa klabu na sote pia, nadhani kuna muda mrefu kabla ya mechi kuamua nani atacheza na nani hatocheza kwenye kile kikosi cha wachezaji 11,” alisema Roberto.


“Kuna wengine tumewaacha, tumemuacha Saido Ntibazonkiza ni mchezaji muhimu sana kwenye kikosi changu, lakini ni majeruhi nitawatumia wachezaji wengine waliokuwepo, ni mchezaji mzuri, lakini wengine watanipa kile ninachokitaka.


Kwa upande wake Sakho alisema kama mambo yatakwenda kama yalivyopangwa basi wanatarajia ushindi kwa sababu lengo si kushinda bali ni kufuzu na kusonga mbele kwenye kundi hilo.


Kocha msaidizi wa Simba, Juma Mgunda amesema kuwa, nyota wa timu hiyo wapo na molari ya hali ya juu kuelekea mchezo wao dhidi ya Horoya na kuhakikisha wanapata ushindi.


Mgunda alisema kuwa, wanatambua uzito wa mechi wanayokwenda kucheza hivyo wamejiandaa kushinda na kudai kuwa morali ya wachezaji ipo juu kuelekea mchezo huo.


"Tunashukuru Mungu kutuwezesha kumaliza vizuri mazoezi ya mwisho tukiwa tunaelekea Guinea, uimara wa wachezaji upo vizuri na tupo tayari kutetea nchi, katika vilabu hivi ndio michuano mikubwa Afrika hivyo hakuna mechi rahisi.


"Ni mechi ambayo itakuwa na uzito mkubwa kwa kutambua hilo tumejiandaa kwenda kukutana na timu ambayo hatujawahi kucheza nayo.


"Kutokana na umuhimu na uzito wa mashindano haya tunachukua tahadhari zote kuhakikisha tunafanya vizuri, kwa hali na morali waliyokuwa nayo wachezaji  tunaamini tutapata ushindi, tunajikabidhi kwa Mwenyezi Mungu," alisema Mgunda.


Post a Comment

0 Comments