Ticker

6/recent/ticker-posts

Jezi Mpya za Simba kuwasili kabla ya mechi ya Raja Casablanca

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Ofisa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba SC, Ahmed Ally amesema kabla ya Februari 18, 2023 mzigo wa jezi mpya utakuwa umefika Tanzania ukitokea Ethiopia ambako umekwama.


Akizungumzia swala hilo la jezi Ahmed Ally amesema jezi hizo zilianza kukwama nchini China hivyo zilifanyika juhudi za kusukuma mzigo huo ili kuachiwa kwa haraka na baada ya kuachiwa ukakwama tena Ethiopia.


“Kutokana na sherehe za mwaka mpya China usafirishaji mizigo ulikuwa wakusuasua ikabidi Vunjabei aende China kuhakikisha jezi hazichelewi ila zikaja kukwama Ethiopia kwasababu ya ndege za mizigo kuchelewa.” Amesema Ahmed Ally.


Amesema kuwa kabla ya mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Raja Casablanca jezi hizo zitakuwa zimefika na kila shabiki atakapata kutokana uwingi wa jezi hizo.


KUHUSU MCHEZO DHIDI YA RAJA CASABLANCA


"Huu ni zaidi ya mchezo wa kawaida ambao mwanadamu amewahi kuona au kufikiria. Sisi kama Simba tunataka jambo moja tu, ni ushindi mbele ya Raja Casablanca”


"Kwa mujibu wa CAF, mchezo ni saa 1:00 usiku, awali tulithibitisha kucheza saa 10:00 jioni lakini ratiba ya mwisho kutolewa na CAF imekuwa saa 1:00 usiku. Tumewaandikia CAF kuwaomba muda wa mchezo uwe saa 10:00 jioni."


"Naomba kuwambia mashabiki wa Simba tuanze kujiandaa na muda wa saa 1:00 usiku. Lakini sisi hatuangalii muda, muda wowote tupo tayari kupambana ili kupata ushindi. Na kama mnakumbuka tulishawahi kucheza saa 4 usiku na tukapata matokeo."


"Waamuzi wa mchezo wanatokea Cameroon. Kuhusu Raja Casablanca tayari tumeshawatumia taarifa kuwauliza watafika lini Tanzania lakini hadi sasa hawajasema lini watakuja."


"Kuhusu Sadio Kanoute hatakuwepo kwenye mchezo unakuja kutokana na kuwa na kadi tatu za njano. Kuhusu Saidi Ntibazonkiza sasa ameshapona, wengine ni Peter Banda."


KUHUSU VIINGILIO KATIKA MCHEZO HUO

"Rais wa heshima wa Simba SC, moodewji kwa mapenzi yake na klabu ya Simba, mapenzi yake na mashabiki wa Simba alituomba tupunguze viingilio. Mzunguko sasa ni Tsh. 3,000, VIP C- Tsh. 10,000, VIP B - Tsh. 20,000 na VIP A - Tsh. 30,000."


"Tumeona taarifa kutoka kwa Msemaji Mkuu wa Serikali, gerson msigwa akitangaza kwamba Rais Mama Samia atanunua kila goli kwa Tsh. 5 milioni."


"Sisi kama Simba kwanza tumefurahi, tunaichukulia kama ni agizo, mama anatutaka tukafunge magoli. Tumepokea na Jumamosi tunamuahidi kufunga magoli mengi kadri iwezekanavyo. Wachezaji wako tayari kumfurahisha mama na kuwafurahisha Watanzania."


"Tunakwenda kwenye mechi kubwa tukijiamini maana tunaamini tunachokwenda kukifanya kwenye michuano hii."


"Ili tuweze kupata matokeo Jumamosi basi mashabiki wa Simba 60,000 tuwaone pale Kwa Mkapa. Wakijaa mashabiki wa Simba hakuna timu Afrika hii inaweza kutoka salama. Tayari tumeanza kuuza tiketi, nunua tiketi yako mapema."- Ahmed ally




Post a Comment

0 Comments