Ticker

6/recent/ticker-posts

Ahmed Ally Awataka Wana Simba kuunganisha nguvu

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally, Amewataka Wanachama na Mashabiki wa Klabu hiyo kuunganisha nguvu ili timu yao Iweze kufanya vizuri katika kipindi hiki kigumu wanacho pitia.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Ahmed Ally amesema Kikosi cha Simba kinataraji kuondoka leo jioni kuelekea Uganda kuwafuata Vipers kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika utakao chezwa Jumamosi hii (February 25).

Ahmed amesema Huu ni mchezo muhimu kwetu, ambao utatoa taswira yetu ya ushiriki wa ligi ya mabingwa msimu huu

Mechi hii inatuhitaji sana na Wana Simba kuunganisha nguvu ili kufanya vizuri

Hatuna option zaidi ya kushikamana na kupambana kila idara ili tupate matokeo yatakayofufua matumaini yetu

Njia pekee ya kufanikiwa kwenye nyakati ngumu ni kuwa wamoja na kufocus mbele

Inawezekana kabisa kuchukua points 3 Uganda lets goo Wana Simba

Majina Ya Wachezaji 24 ambao watasafiri leo jioni kwenda Uganda.

WACHEZAJI SIMBA WAOMBA RADHI KWA MASHABIKI

NAHODHA wa Simba, John Bocco ameomba radhi kwa mashabiki wa timu hiyo kwa kushindwa kupata ushindi kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Tanzania Bara.

Bocco ameeleza kuwa uchovu na kukosa muda wa kutosha wa mapumziko ni moja ya sababu iliyofanya wasing’are, lakini bado hawajakata tama.

“Ni matokeo mabaya ambayo yanawaumiza mashabiki wetu, lakini hata sisi wachezaji hatuyafurahii, tunaomba watuvumilie na kutuunga mkono sababu ni jambo la mpito,” amesema Bocco.

Sare dhidi ya Azam FC, imeifanya timu hiyo kupitwa pointi nane dhidi ya vinara wa ligi hiyo Yanga.


Mangungu awashukia Waandishi wa Habari kuwa chanzo cha migogoro ndani ya Klabu hiyo

Post a Comment

0 Comments