Ticker

6/recent/ticker-posts

Aguero awaponda Arsenal, asema EPL itaenda Manchester United au City

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Aliyekuwa mshambuliaji matata wa timu ya Manchester City, Muargentina Sergio Kun Aguero ametoa tamko ambalo limechefua mioyo ya mashabiki wengi wa Arsenal.


Aguero anahisi kuwa bado ni mapema sana kwa mtu yeyote kuweka matumaini kwa Arsenal kuchukua Ubingwa wa mwaka huu, huku akisema kuwa timu kama Manchester City, United na Newcastle wapo na nafasi kubwa ya kushinda taji hilo kuliko Arsenal.


Arsenal mpaka sasa wanashikilia usukani kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya premia Uingereza kwa alama zaidi ya tano baada ya mechi za mzunguko wa 19, Aguero bado anahisi kuwa hawafai kupewa nafasi moja kwa moja kuwa ndio mabingwa watarajiwa.


“Kwa jinsi mambo yalivyo, itaenda kwa Arsenal, City au United," gwiji huyo wa City Aguero alisema. "Newcastle pia haiwezi kupunuzwa. Wamecheza vizuri mzunguko wa kwanza wa michuano hiyo.”


Vijana wa Mikel Arteta kwa sasa wako kileleni mwa msimamo wakiwa na pointi 50 na wana faida ya pointi tano zaidi ya Manchester City inayoshika nafasi ya pili. Arsenal wamepoteza mara moja pekee kwenye ligi ya ndani katika mechi 19 walizocheza, huku kichapo chao pekee kikiwa cha mwezi Septemba mikononi mwa wapinzani, Man United.


Arsenal haijashinda Ligi ya Premia tangu wahamie kwenye Uwanja wa Emirates mwaka 2006, huku mataji yao matatu yote yakiibuka wakicheza kwenye uwanja wao wa zamani wa Highbury.


Post a Comment

0 Comments