Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga yazindua jezi maalum kwajili ya mashindano ya Kombe la Shirikisho la CAF

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Klabu ya Yanga imezindua jezi maalum ambazo itazitumia kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho la CAF [CAF Confederation Cup] 2022|23 kuanzia hatua ya Makundi.


Ukiangalia jezi hizo mpya, kifuani amewekwa mdhamini ambaye wamemtangaza leo, kampuni ya Haier zina kwa sababu mdhamini mkuu wa Yanga [kampuni ya michezo ya kubahatisha] hawataweza kumtumia kwenye mashindano ya CAF kuanzia hatua ya makundi.

"Yanga imeingia mkataba na kampuni ya Haier wenye thamani ya Tsh bilion 1.5 kama mdhamini mkuu wa Kombe la shirikisho barani afrika" Rais Hersi Ally Said 
jezi hizi zinapatikana Duka la Yanga Makao Makuu pekee kwa gharama ya shilingi elfu 50,000


Taratibu za masoko za CAF haziruhusu timu yoyote kuvaa jezi yenye mdhamini wa kampuni ya kubahatisha kwakuwa tayari CAF inadhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha [wanazuia mgongano wa kimaslahi].

Ndio maana misimu kadhaa nyuma, Simba ilicheza huku jezi zao zikiwa hazina mdhamini kifuani lakini baadae wakaja na Visit Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Utalii ili kutangaza utalii wa Tanzania.


HAIER INAJIHUSISHA NINI?

Haier ni kampuni ya kimataifa inayoshikilia rekodi ya ubora ya uzalishaji wa bidhaa za nyumbani ‘home appliances’ [TV, Fridge, AC, Washing Machines, Cookers, Microwaves n.k].


Wanashikilia rekodi ya maiaka 14 ya ubora duniani na uvumbuzi na wamekuja Tanzania kuhudumia soko la hapa.Post a Comment

0 Comments