Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Jumapili 15.01.2023

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Barcelona hawana haraka ya kumuuza mshambuliaji wa Uholanzi Memphis Depay na wana furaha kumbakisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 hadi mkataba wake utakapokamilika msimu wa joto. (Athletic)


Real Madrid wanamfanya kiungo wa kati wa Uingereza na Borussia Dortmund Jude Bellingham, 19, kuwa kipaumbele katika soko la usajili. (Fichajes - in Spanish)


Chelsea wametenga dau la euro 30m (£26.5m) kumnunua winga wa PSV Eindhoven wa England chini ya umri wa miaka 21 Noni Madueke, 20. (ESPN).


Liverpool wamemaliza mazungumzo ya kandarasi na kiungo wa kati Naby Keita na watamruhusu mchezaji huyo wa kimataifa wa Guinea, 27 kuondoka kwa uhamisho wa bure msimu wa joto. (Football Insider)


Chelsea walikuwa na ofa ya mkopo kwa mshambuliaji wa Jamaica Michail Antonio, 32, iliyokataliwa na West Ham. (Guardian)


Everton wanataka kumsajili winga wa Uswidi Anthony Elanga mwenye umri wa miaka 20 kutoka Manchester United. (Football Insider)


Crystal Palace wanahofia gharama za kumsajili beki wa kulia Muingereza Aaron Wan-Bissaka kutoka Manchester United, 25. (Sun)


Tottenham watakutana na Sporting Lisbon wiki hii kujadili kuhusu dili la beki wa kulia wa Uhispania Pedro Porro, 23, ambaye amekubali masharti binafsi na klabu hiyo. (Mirror)


Tottenham wanapanga kumnunua beki wa Bayer Leverkusen na Ecuador Piero Hincapie, 21 kwa pauni milioni 20. (Sun)


Wolves wana nia ya kumnunua beki wa kati wa Newcastle Jamaal Lascelles, 29, ikiwa hawataweza kumsajili Craig Dawson mwenye umri wa miaka 32 kutoka West Ham. (Football Insider)


Nottingham Forest wanakaribia kumsajili kiungo wa kati wa Palmeiras Mbrazili Danilo, 21. (90min).


Mshambuliaji wa Villarreal na Uholanzi Arnaut Danjuma, 25, yuko London kufanya mazungumzo na vilabu, ikiwa ni pamoja na Bournemouth, kuhusu uhamisho wa mkopo wa Januari. (Athletic)


Bournemouth wanatayarisha mkataba wa pauni 50,000 kwa wiki ili kumjaribu mshambuliaji wa Ghana Antoine Semenyo mwenye umri wa miaka 23 kutoka Bristol City. (Sun)


Southampton wanataka kusajili nyota wawili wa shule ya Manchester City - kiungo Kian Breckin, 19, na winga wa Ureno mwenye umri wa miaka 18 Carlos Borges. (Sun)


TETESI ZA USAJILI MPYA SIMBA SC


Post a Comment

0 Comments