Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba Wamtambulisha Imani Kajula Kuwa CEO Wao Mpya

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Klabu ya Simba  imemtambulisha Imani Kajula kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa klabu hiyo kwa mkataba wa miezi sita, akichukua nafasi ya Barbara Gonzalez aliyejiuzulu.


Kajula ni mzoefu kwenye uongozi wa mpira kwani alikuwepo kwenye Kamati ya maandalizi ya Michuano ya Afrika ya vijana chini ya umri wa miaka 17 yaliyofanyika nchini mwaka 2019.


Kwa mujibu wa Meneja wa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema mkataba huo unaweza kurefushwa endapo Bodi itaridhishwa na utendaji wake katika kipindi cha miezi sita waliyompatia hivi sasa.


Kajula ni mbobevu wa masuala ya Masoko na Mawasiliano na amefanya kazi na makampuni mbalimbali na mabenki ndani na nje ya nchi.


Miongoni mwa kazi alizofanya mpaka sasa.


– Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano NMB (2006-2013)


– Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Posta (2003-2006)


– Meneja Masoko wa CRDB (1999-2003)


Akiwa EAG Group Kajula alikuwa sehemu ya maandalizi ya Wiki ya Simba mpaka kilele chake (Simba Day) ambapo kampuni hiyo ndiyo ilitengeneza mitandao ya kijamii ya klabu.


Post a Comment

0 Comments