Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba Kushusha Mashine Ya Hatari

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally ameeleza kuwa timu hiyo inaendelea na mchakato wa usajili na itaendelea kuimarisha sehemu ya ushambuliaji na eneo la ulinzi.


Akizungumza asubuhi hii na kituo kimoja cha redio, Meneja huyo amesema licha ya ushindi wanaoupata, lakini eneo la ushambuliaji linahitaji nguvu zaidi ili kuendelea kuongeza idadi ya mabao.


Amesema timu hiyo inakusudia kumtangaza mchezaji mwenye kiwango bora kumzidi Saido Ntibazonkiza aliyesajiliwa hivi karibuni akitokea Geita Gold na kufunga mabao matatu katika mchezo wake wa kwanza wa ushindi wa mabao 7-1 dhidi ya Tanzania Prisons.


“Wanasimba wasiwe na wasiwasi kuna mchezaji hatari tunamalizana naye, tutamsajili mchezaji hatari zaidi ya Saido Ntibazonkiza tuliyemtangaza hivi karibuni, wanasimba mtafurahi,” amesema Ahmed Ally.


Kwenye safu ya ulinzi wa Simba imeruhusu mabao tisa, Ahmed Ally anasema timu hiyo ina lengo la kuboresha eneo hilo kwenye usajili wa dirisha dogo lengo likiwa kupunguza idadi ya mabao ya kufungwa.


Post a Comment

0 Comments