Ticker

6/recent/ticker-posts

Musonda Awaahidi Makubwa Wanachama na Mashabiki Wa Yanga

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Mshambuliaji mpya wa Yanga raia wa Zambia, Kennedy Musonda, amewaahidi wanachama na mashabiki wa timu hiyo mabao zaidi kwenye michuano mbalimbali ambayo atacheza.


Musonda alisema hayo baada ya kufunga mabao mawili kwenye mechi ya 32 bora ya Kombe la FA dhidi ya Rhino Rangers kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo tangu ajiunge na klabu hiyo siku kadhaa zilizopita kwenye kipindi cha dirisha dogo.


Mabao yangu yote  mazuri, lakini nimelipenda la kwanza na ukiwa kwenye timu kubwa kama hii ni lazima kichwa kitulie, kwa sababu ina wanachama na mashabiki wengi ambao wanategemea kitu kutoka kwako.


Namshukuru Mungu nilikuwa na presha ya kufunga mabao, nina furaha nimefunga mabao haya ambayo yamenipa kujiamini na sasa naamini mabao mengi yatakuja.


Nawaahidi Wanayanga mabao zaidi, ushindi na mchezo bora," alisema Musonda baada ya kufunga mabao mawili .


Alisema pamoja na kuwa na hamu ya kufunga, lakini hakuwa na wasiwasi sana na lilikuwa ni suala la muda tu yeye kufanya hivyo.


"Unajua mshambuliaji unapokuwa uwanjani unatarajia muda wowote utafunga, lakini kama hukupata bao unatakiwa uamini tu kuwa mechi ijayo utafunga," alisisitiza.


Ilimchukua dakika 16 kupachika bao lake la kwanza kwenye mechi hiyo, likiwa la pili kwenye mchezo, lingine akifunga dakika ya 46.


Mabao mengine kwenye mechi hiyo ambayo Yanga ilishinda mabao 7-0, yalifungwa na Dickson Ambundo, Stephane Aziz Ki, Farid Mussa, Yannick Bangala, na David Brayson.


Musonda ambaye alisajiliwa na Yanga kipindi cha dirisha dogo la usajili akitokea klabu ya Power Dynamos ya Zambia, hakufunga kwenye mechi mbili za mwanzo za Ligi Kuu ambazo timu yake ilicheza, akiingia kipindi cha pili kwenye mechi dhidi ya Ihefu Januari 26 ambapo ilishinda bao 1-0, na alianza kwenye mechi ambayo Yanga ilicheza dhidi ya Ruvu Shooting na kushinda bao 1-0, mechi zote zikicheza kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.


Kutofunga bao lolote kwenye mechi hizo mbili kulianza kuleta minong'ono kwa baadhi ya mashabiki wa soka. 


Habari Kubwa Za Magazeti Ya Leo January 28 2023Post a Comment

0 Comments