Ticker

6/recent/ticker-posts

Manchester City Kuwavaa Tottenham Hotspur Leo

 

BAADA ya kupoteza mechi za debi mwishoni mwa wiki, Manchester City na Tottenham Hotspur leo Alhamisi watashuka katika dimba la Etihad kuzitafuta pointi tatu katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).


Man-City ya Pep Guadiola walichapwa mabao 2-1 na Manchester United katika dimba la Old Trafford mnamo Jumamosi, siku moja kabla ya Spurs kufugwa na Arsenal mabao 2-0 katika uwanja wao wa nyumbani.


Guardiola amesema mawazo yake hayako kwa ubingwa wa EPL msimu huu, ingawa kikosi chake kinaendelea kupambana na Arsenal ya kocha Mikel Arteta kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) .


Kufikia sasa, mabingwa watetezi wa EPL, Man-City, wanakamata nafasi ya pili wakiwa na alama 39, nane nyuma ya Arsenal ambao wamecheza mechi 18.


Kwa upande wake, kocha Antonio Conte wa Spurs amesema hafai kulaumiwa kutokana na matokeo duni ya timu hiyo.


Conte amedai kuna watu wengine wanaopaswa kubeba mzigo huo wa lawama baada ya timu kushindwa mara tano katika mechi tisa za ligi.


Licha ya Spurs kushuka hadi nafasi ya tano katika msimamo, Conte amesisitiza kuwa hajaona maafisa wengine wa klabu hiyo wakiwemo madaktari na wakurugenzi wa idara ya michezo wakilalamika kuhusu mfumo unaotumiwa kwa sasa.


“Nchini Italia, kabla ya mechi kuanza, kuna mtu anayezungmza na waandishi wa habari. Hapa pia inafaa iwe hivyo, lakini imekuwa ni mimi tu ninayeeleza kila kitu, hivyo sioni kama ni sawa.”


“Wakati umefika kwa wakuu wa klabu kuwakilishwa katika mikutano ya pamoja na waandishi wa habari kueleza kinachoendelea kikosini kwa sasa, la si hivyo, itaonekana kuna jambo linalofichwa, ambalo linaendelea kutuvuruga,”akaelezea.


Spurs wamepata pointi 10 pekee katika mechi tisa zilizopita.


Pengo la alama tano linatamalaki kati yao na Manchester United na Newcastle United ambao wapo mbele kwa mchezo mmoja dhidi ya Spurs


“Nionavyo, kila mtu anatia bidii uwanjani, lakini imekuwa vigumu kushinda. Kibarua ni kizito na matarajio ni mengi,” alisema kocha huyo wa zamani wa Chelsea.


Tetesi Za Soka Barani Ulaya January 19,2023


Post a Comment

0 Comments