Ticker

6/recent/ticker-posts

Kocha Mpya Simba Aahidi Ubingwa Wa Afrika

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Kocha Mkuu wa Simba Mbrazil Roberto Oliviera ‘Robertinho amesema malengo yake msimu huu ni kuchukua ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika akiwa na timu hiyo.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 21,2023, jijini Dodoma, kocha huyo aliyeichukua Simba mwanzoni mwa mwezi huu akitokea Vipers ya Uganda, amesema malengo aliyojiwekea ni kuchukua ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika na hilo linawezekana kwani ana wachezaji wenye uwezo mkubwa.


“Tunataka kuchukua ubingwa wa Tanzania na ubingwa wa klabu bingwa Afrika, kwanini tusichukue wakati tuna timu bora,”amesema kocha huyo.


Kocha huyo amesema walikuwa na kambi nzuri Dubai na wamecheza michezo kadhaa ya kirafiki iliyosaidia kukiweka vizuri kikosi chake.


Amesema kubwa kwa sasa ni kuhakikisha timu inapata pointi tatu kama ilivyokuwa katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City.


Post a Comment

0 Comments