Ticker

6/recent/ticker-posts

Kocha Erik Ten Hag Awaonya Arsenal

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Kocha wa Manchester United Erik ten Hag amekataa kutishwa na uhalisia na amewaonya Arsenal dhidi ya kusherehekea kuwa Casemiro atakosa mechi yao ya Jumapili hii katika dimba la Emirates. 


Katika mahojiano mnamo Alhamisi - Januari 19, ten Hag alisema kuwa United ilisajili ushindi dhidi ya Arsenal katika mkondo wa kwanza bila Casemiro na watahitajika kulirudia hilo. 


"Tuliwapiga bila Casemiro - sasa tunahitajika tena kufanya vivyo hivyo," Ten Hag alisema. 


Casemiro alicheza tu kwa dakika kumi katika ushindi wa 3-1 wa United dhidi ya Arsenal Septemba mwaka jana na hatacheza mechi ya Jumapili baada ya kujilimbikizia kadi tano za manjano. 


Raia huyo wa Brazil alipewa kadi ya manjano katika dakika ya 80 katika mechi dhidi ya Crystal Palace mechi ambayo United waliambua sare ya 1-1 licha ya kuongeza hadi dakika ya 90. 


Palace walikuwa wanatishia kupata goli kila mara hususani katika kipindi cha pili na Casemiro hakuwa na budi ila kumchezea rafu Wilfried Zaha alipokuwa akitimka kuelekea kwa lango la United na mpira. 


"Yeye ni mchezaji muhimu sana kwetu na moja ya sababu ya sisi kuwa katika nafasi hii. Tunashinda, tunadhibiti mechi kisha bahati mbaya inatokea. Tunafaa kulikubali na kusonga mbele na tuunde mbinu bora zaidi kwa ajili ya Arsenal," kocha huyo aliongeza. 


Casemiro kwenye umri wa miaka 30 amekuwa nguzo katika kikosi cha Manchester United tangu kujiunga mwanzoni mwa msimu akitokea Real Madrid. The Red Devils wamepoteza tu mechi moja kati ya 20 zilizopita katika mashindano yote na sasa wanashikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo la Ligi Kuu ya Uingereza. 


Simba Yashusha Kocha Msaidizi Kutoka Tunisia
Post a Comment

0 Comments