Ticker

6/recent/ticker-posts

Jurgen Klopp - Sina mpango wa kuondoka Liverpool

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa



KOCHA Jurgen Klopp amesema hana mpango wowote wa kuondoka Liverpool iwapo hatalazimishwa kufunga virago.


Hata hivyo Klopp, amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitayarisha kwa mabadiliko makubwa ndani ya Anfield mwishoni mwa msimu huu wa 2022-23.


Klopp ametoa kauli hiyo baada ya mabosi wake kuanza kushangazwa na msururu wa matokeo mabovu msimu huu. Kufikia sasa, Liverpool wanakamata nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) huku pengo la alama 10 likitamalaki kati yao na Manchester United waliopo nafasi ya nne.


“Huenda awe ni kocha ataondoka au mabadiliko hayo yashuhudiwe kikosini. Madiliko lazima yawepo japo sioni nikiagana na Liverpool iwapo sitaondoshwa na mtu,” amesema kocha huyo raia wa Ujerumani.


Kwa mujibu wa Klopp, Liverpool hawatamsajili mchezaji yeyote mwingine Januari 2023 baada ya kujinasia huduma za fowadi mzoefu raia wa Uholanzi, Cody Gakpo. Kubwa zaidi katika mipango ya Liverpool ni kurefusha mikataba ya James Milner, Naby Keita, Alex Oxlade-Chamberlain na Roberto Firmino. Kandarasi za wanne hao zinatamatika rasmi mwishoni mwa msimu huu.


Kichapo kutoka kwa Brighton kiliacha Liverpool katika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa EPL kwa pointi 28 sawa na Chelsea itandika Crystal Palace bao 1-0 katika dimba la Stamford Bridge, Jumapili.


Liverpool sasa hawajashinda mechi tatu mfululizo katika mashindano yote. Wamefungwa mabao manane katika kipindi hicho na hawajawahi kuondoka bila kufungwa bao katika michuano saba.


Mabingwa hao watetezi wa Kombe la FA wamewahi kuondolewa kwenye raundi ya tatu ya kipute hicho mara moja pekee katika kipindi cha misimu 11 iliyopita. Hiyo ilikuwa mikononi mwa Wolves mnamo 2018-19, mwaka mmoja baada ya Wolves kuwadengua kwenye raundi ya nne mnamo 2016-17.


Tangu Wolves wapokeze Liverpool kichapo cha 2-1 katika Kombe la FA mnamo 2019 ugani Molineux, masogora wa Jurgen Klopp walishinda mechi saba mfululizo dhidi ya mbwa-mwitu hao katika EPL hadi walipoambulia sare mwezi huu.


Post a Comment

0 Comments