Ticker

6/recent/ticker-posts

De Gea Akasirika Baada Ya Casemiro Kupigwa Marufuku Kucheza Dhidi Ya Arsenal

 

KIPA wa Manchester United David De Gea ametoa povu baada ya kiungo Casemiro kupigwa marufuku ya kucheza dhidi ya Arsenal siku ya Jumapili katika dimba la Emirates.


De Gea anashangaa mbona United walipangiwa mechi katikati ya wiki - siku nne tu kabla ya mechi yao na Arsenal - ilhali wenzao hawakuwa na mechi katikati ya wiki. 


Katika sare hiyo ya 1-1 na Crystal Palace, kiungo matata Casemiro alipata kadi ya manjano na kufungiwa nje ya mechi hiyo ya Arsenal jambo ambalo limemghadhabisha De Gea. 


Pigo kubwa kukosa Casemiro Jumapili. Sielewi mbona Arsenal hawechezi katikati ya wiki ilihali sisi tunacheza. Sasa tunakosa mmoja wa wachezaji wetu muhimu. Sielewei. Sasa tunamkosa kwa mechi kubwa na ni pigo kubwa kwetu, De Gea alisema.


Casemiro alipewa kadi ya manjano katika dakika ya 80 ugani Selhurst Park kwa kumchezea rafu Wilfried Zaha alipokuwa akitimka kuelekea kwa lango la United na mpira na uwezekano wa kusawazisha. 


Ten Hag: Tulipiga Arsenal bila Casemiro 


Kocha wa United Erik ten Hag hata hivyo amekataa kutishwa na uhalisia wa Casemiro kukosa mechi hiyo baada ya kujilimbikizia kadi tano za manjano. 


ten Hag alisema kuwa United ilisajili ushindi dhidi ya Arsenal katika mkondo wa kwanza bila Casemiro na watahitajika kulirudia hilo. 


Tuliwapiga bila Casemiro - sasa tunahitajika tena kufanya vivyo hivyo, Ten Hag alisema.


Casemiro alicheza tu kwa dakika kumi katika ushindi wa 3-1 wa United dhidi ya Arsenal Septemba mwaka jana. Post a Comment

0 Comments