Ticker

6/recent/ticker-posts

Chama Mchezaji Bora Wa Mashabiki Simba

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Kiungo kutoka nchini Zambia Clatous Chotta Chama ametajwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Simba SC kwa mwezi Disemba, 2022.


Chama ameibuka kidedea akiwashinda Beki Shomari Kapombe na Mshambuliaji John Bocco, ambao alikuwa ameingia nao fainali kwenye kinyang’anyiro hicho.


Katika mwezi Desemba 2022, Chama alicheza Dakika 540 akifunga mabao manne na kusaidia Simba SC kupatikana kwa mengine saba.


Mashabiki 3,355 wa Simba SC walipiga Kura katika Kinyang’anyiro hicho na Chama amepata Kura 1829 sawa na asilimia 54.52.


Mshambuliaji John Bocco ameshika nafasi ya pili, baada ya kupata Kura 1415 sawa na asilimia 42.18, huku Beki Shomari Kapombe akishika nafasi ta tatu kwa kupata Kura 111 sawa na asilimia 3.31.


Cesar Manzoki Kukamilisha Usajili Simba Muda WowotePost a Comment

0 Comments