Ticker

6/recent/ticker-posts

Arsenal Waendeleza Ubabe Wao Emirates, Waitandika Man United 3-2

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Arsenal Waendeleza Ubabe Wao Emirates, Waitandika Man United 3-2

Mjadala wa ni mkali kati ya Arsenal na Manchester United umefika kikomo baada ya mechi iliyopigwa hapo jana (january,22) katika uwanjani Emirates kumalizika kwa Man United kukubali kichapo cha Mabao 3-2 dhidi ya Arsenal.


Manchester United, maarufu kama mashetani wekundu, ndio walikuwa wa kwanza kuona lango lakini kufikia kipenga cha mwisho kupuulizwa walijua kutangulia baa si kulewa. 


Marcus Rashford ndiye alikuwa wa kwanza kucheka na nyavu dakika ya 17 kipindi cha kwanza lakini kabla hata wino ulioandika bao hilo kukauka Eddie Nketiah akaisawazishia Arsenal. 


Arsenal walichukua usukani baada ya Bukayo Saka kuandikia Arsenal bao la pili lakini Man United wakapambana mbaka Lisandro Martinez alipo wasawazishia.


Hata hivyo, bao la Nketiah dakika za lala salama lilitosha kuwarudisha Man United nyumbani wakiwa wamekunja mkia. 


Sasa ushindi huo muhimu kwa Arsenal umewaweka kileleni na pointi 50 huku nia yao ya kushinda kombe la Premier ikiongezeka. 


Post a Comment

0 Comments