Ticker

6/recent/ticker-posts

Arsenal Kumnasa Trossard Kutoka Brighton Hove Albion Muda Wowote

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Arsenal wapo katika hatua nzuri tayari kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji Leandro Trossard kutoka Brighton Hove Albion.


Taarifa ya mwandishi wa habari za michezo kutoka nchini Italia, Fabrizio Romano imeeleza kuwa makubaliano baina ya mchezaji huyo na Arsenal yameafikiwa huku mazungumzo baina ya timu hizo yakiendelea ili kukamilisha usajili huo.


Arsenal imemgeukia mchezaji huyo baada ya chaguo lao la kwanza Mykhailo Mudryk kusajiliwa na Chelsea hata hivyo zipo tetesi kuwa Chelsea pia inamhitaji mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji.


Wiki moja iliyopita wakala wa mchezaji huyo, Josy Comhair alitoa taarifa ya hali ilivyo kwa mchezaji wake baada ya kuingia kwenye mgogoro na kocha wa Brighton Roberto De Zerbi.


Taarifa ya Comhair ilieleza kuwa “Kabla ya Leandro kwenda Qatar(World Cup 2022) ilikuwa nia ya Brighton kumuongezea mkataba, hili halikufanyika kwa vile pande zote hazikufikiana. Leandro pia ameonyesha yuko tayari kwa hatua inayofuata.”


“Baada ya Kombe la Dunia kulikuwa na ugomvi kwenye mazoezi kati ya Leandro na mchezaji mwingine. Tangu wakati huo, kocha hajazungumza na Leandro, kitu ambacho hakifai na dhahiri hakina afya kwa mazingira ya mchezaji.” ilieleza taraifa ya wakala huyo.


Taarifa yake iliendelea kufafanua kuwa “Leandro bado alikuwa mchezaji miongoni mwa waliotakiwa kucheza dhidi ya Southampton na Arsenal lakini dhidi ya Everton alikuwa kwenye benchi. Katika mabadiliko matano yaliyofanyika wakati huo, pia hakuwa miongoni mwao na hii haina maelezo yoyote.” ilifafanua taarifa yake.


“Katika maandalizi ya mechi dhidi ya Middlesbrough Kombe la FA, Leandro alilipoti kuwa na tatizo hii ndiyo sababu iliyomfanya aache mazoezi. Hii ilikuwa kwa kushauriana na wahudumu wa afya.”ilieleza taarifa yake.


Jumatatu iliyopita kocha De Zerbi alisema kuwa hataki kumuona tena mchezaji huyo mazoezini hata hivyo mchezaji huyo amekuwa akifanya mazoezi peke yake, licha ya kuambiwa asiwepo kwenye kikosi cha Brighton.


Kocha huyo alisema tabia za mchezaji huyo zimemfanya kuchukua maamuzi hayo kwani mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Middlesbrough aliondoka mazoezini bila kumwambia chochote kocha wake tabia ambayo kocha wake alisema ni mbovu.


Post a Comment

0 Comments