Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga kusajili watatu dirisha dogo

Kocha wa Yanga Nasreddine Nabi, amesema Yanga itasajili wachezaji watatu pekee kwenye dirisha dogo ambalo linatarajiwa kufunguliwa kuanzia tarehe 15 mwezi huu wa Desember 2022.

Akizungumza na SpotiLeo, kocha huyo amesema hiyo ni kutokana na mapungufu machache aliyoyaoba kwenye kikosi chake baada ya mechi za mtoano na mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Hatuitaji kufanya usajili wa wachezaji wengi sababu bado tuna timu nzuri ya ushindani hao wachezaji watatu ambao tumepanga kuwaongeza kwenye dirisha dogo ni kwa ajili ya kuziba sehemu zilizoonesha mapungufu kwenye mechi za mtoano na ligi,” amesema Nabi.

Kocha huyo amezitaja nafasi ambazo wataziboresha kuwa ni beki mmoja wa kati, mshambuliaji mmoja na kiungo mkabaji.

Katika droo ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika Yanga imepangwa kundi D na timu za TP Mazembe, AS Bamako na US Monastir ya Tunisia.

Post a Comment

0 Comments