Ticker

6/recent/ticker-posts

Ujerumani Yatupwa Nje ya Kombe la Dunia Katika Hatua ya Makundi

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Timu ya taifa ya Ujerumani imetupwa nje ya  mashindano ya Kombe la Dunia nchini Qatar katika hatua ya makundi licha ya kapata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Costa Rica katika mchezo wa mwisho wa kundi E  - hii ikiwa mara ya pili mfululizo. 

Nini kilitokea hadi Ujerumani kuondoka? 

Ujerumani imeaga mashindano ya 22 ya Kombe la Dunia licha ya kufanya walichohitajika kufanya katika mechi yao ya mwisho - kupata ushindi dhidi ya Costa Rica. 

Ujerumani imeibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Costa Rica - Serge Gnabry, Kai Havertz (mawili) na Niclas Fullkrug wakiwa wafungaji. 

Hata hivyo licha ya kupata ushindi huu, hawakuwa na uhakika kuwa wangefuzu kwa hatua ya 16 kwani walitegemea Uhispania kuifunga Japan ili na wao wafudhu. 


Nini kilitokea katika mechi ya Uhispania na Japan? 

Alvaro Morata aliipa Spain uongozi katika dakika ya 11 ya mchezo na kuchochea sherehe katika kambi ya Ujerumani kwani mambo yalikuwa yanaenda walivyotamani. 

Hata hivyo Ao Tanaka na Ritsu Doan walicheka na wavu katika kipindi cha pili na kuipa Japan ushindi wa 2-0 dhidi ya mabingwa wa mwaka 2010. 


Msimamo wa kundi E 

Japan wamefuzu kwa raundi ya 16 kama viongozi wa kundi E kwa alama sita baada ya ushindi katika mechi zao dhidi ya Ujerumani na Uhispania. 

Uhispania imekuwa ya pili kwa alama nne na ubora wa mabao huku Ujerumani na Costa Rica zikiondoka katika nafasi ya tatu na nne. 

Baada ya kushinda makala ya mwaka 2014 nchini Brazil, Ujerumani sasa imeondoka katika hatua ya makundi mara mbili mfululizo - 2018 nchini Urusi na 2022 nchini Qatar.

Post a Comment

0 Comments