Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za Soka barani Ulaya Jumatatu 26.12.2022

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Manchester City wamedhamiria kushinda katika ushindani wa kumnunua Jude Bellingham wa Borussia Dortmund na wanaamini kuwa kiungo huyo wa kati wa Uingereza, 19, atakataa uhamisho wa pauni milioni 100 kwenda Real Madrid au Liverpool ili kufanya kazi na kocha wa City Pep Guardiola. (Sun)


Manchester United imeanza mazungumzo na PSV Eindhoven kuhusu kumsajili winga wa Uholanzi Cody Gakpo, 23. (Mirror)


Al-Nassr wanatumai watakamilisha usajili wa mshambuliaji wa Ureno na mchezaji huru Cristiano Ronaldo, 37, kabla ya dirisha la uhamisho la Januari kufunguliwa. (CBS Sports)


Manchester United wanaamini kuwa wana nafasi ya hatimaye kumsajili Frenkie de Jong msimu ujao, lakini wanahisi Barcelona wanajaribu kuongeza thamani yake kwa kusema kiungo huyo wa kati wa Uholanzi, 25, hauzwi. (Sport - in Spanish)


Newcastle wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Borussia Monchengladbach na Ufaransa Marcus Thuram, 25. (Times)


Barcelona hawana nia ya kumuuza kiungo wao wa kati wa Ivory Coast Franck Kessie, 26, au beki wa kulia wa Uhispania Hector Bellerin, 27, mnamo mwezi Januari. (Fabrizio Romano)


Paris St-Germain wana nia ya kumleta winga wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 26 Marco Asensio, ambaye amekuwa akihusishwa na Arsenal. (Sport - in Spanish)


PSG pia inamtaka kiungo wa kati wa Manchester United na Brazil Fred, licha ya klabu hiyo ya Old Trafford kuanza tena masuala ya  nyongeza ya miezi 12 kwenye kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (Sun)


Chelsea wanakaribia kukamilisha mazungumzo ya kumnunua mshambuliaji wa Molde na Ivory Coast David Datro Fofana, 20, na kiungo wa kati wa Vasco da Gama Mbrazil Andrey Santos, 18. (Standard)


DC United wamefikia makubaliano ya mdomo kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati wa Leeds na Poland Mateusz Klich, 32. (MLSsoccer.com, via Mail)


Mwenyekiti wa Crystal Palace Steve Parish anasema klabu hiyo inalenga kufanya usajili wa mkopo mwezi Januari, badala ya kuleta wachezaji kwa mikataba ya kudumu. (Athletic - subscription required)


AC Milan wako tayari kukutana na Rafael Leao, ambaye mkataba wake unaendelea hadi 2024, na kumpa mkataba mpya wenye thamani mara tano ya mshahara wake wa sasa. Timu hiyo ya Italia inataka kumfanya mshambuliaji huyo wa Ureno, 23, kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi ili kuzuia nia yake ya kutaka kuondoka klabuni hapo. (Corriere della Sera, via AS)Mshambulizi wa Ujerumani Youssoufa Moukoko, 18, amekiri ‘’alishtuka’’ kuona ripoti kwamba madai yake ya mshahara yamesababisha mvutano wa kandarasi na Borussia Dortmund. (90min)


Winga wa Brazil, Tete, ambaye amesajiliwa na Shakhtar Donetsk lakini yuko kwa mkopo Lyon, anaweza kufanya uhamisho wa kudumu Januari. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 pia amepewa ofa na vilabu kadhaa vya Premier League. (90min)


Arsenal wapo mbioni kumwongezea mkataba  kiungo wa kati Charlie Patino, 19, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Blackpool. (Standard)


Tetesi za Soka Barani Ulaya Ijumaa 23.12.2022

Post a Comment

0 Comments