Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za Soka Barani Ulaya Ijumaa 23.12.2022

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham anapendelea kujiunga na Real Madrid kutoka Borussia Dortmund, licha ya Liverpool, Manchester City na Manchester United kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19.(AS - kwa Kihispania)


Benfica imekataa ofa ya euro milioni100 (£88m) kutoka kwa klabu ambayo haijatajwa jina kwa ajili ya kiungo wa kati wa Argentina Enzo Fernandez, ambaye amekuwa akihusishwa na Liverpool na Real Madrid, na haitamuuza kwa chini ya euro milioni 120 mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 (£106m). (Record - kwa Kireno)


Real Madrid wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Italia Manuel Locatelli, 24, ambaye yuko kwa mkopo Juventus kutoka Sassuolo, ikiwa watamkosa Bellingham au Fernandez. (AS - kwa Kihispania)


Chelsea wamefikia mkataba wa euro milioni12 (£10.5m) na Molde ili kumsaini mshambuliaji wa Ivory Coast David Datro Fofana, 20. (Fabrizio Romano).


Mlinda mlango wa Chelsea na Senegal Edouard Mendy, 30, amepuuzilia mbali mkataba mpya wa miaka sita Stamford Bridge kwa sababu anaamini kuwa klabu hiyo haimuonyeshi "heshima" ya kutosha linapokuja suala la mshahara. (Sun)


Afisa mkuu mtendaji wa Shakhtar Donetsk Carlo Nicolini amethibitisha kuwa Arsenal wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Ukraine Mykhailo Mudryk, 21. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)


Arsenal wanajaribu kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 27, ambaye kandarasi yake itamalizika Juventus msimu wa joto. (Repubblica, via Mail)


Arsenal bado hawajaamua iwapo watamruhusu mlinzi wa Ureno Cedric Soares kuondoka mwezi Januari, huku Fulham wakiongoza mbio za kumsaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye pia anawavutia Bayer Leverkusen na Villarreal. (Evening Standard)


Mshahara wa kila wiki wa Soares wa karibu £75,000 umekuwa kizingiti. (Sun)


Post a Comment

0 Comments