Ticker

6/recent/ticker-posts

TANZIA: WANASOKA Watuma Salamu Za Pole Kufuatia Kifo Cha Pele

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 MWANASOKA raia wa Brazil aliyejizolea sifa tele kwa weledi wake, Edson Arantes do Nascimento almaarufu Pele, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.


“Kitu kizuri kutoka kwetu ni kukupongeza. Tunakupenda sana. Pumzika kwa amani,” bintiye Pele, Kely Nascimento ameandika kwa Instagram.


Pele licha ya kustaafu mwaka 1977 jina lake limesalia vinywani mwa wachanganuzi wa soka wakimtunuka sifa kama mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea. Aliisaidia Brazil kutwaa Kombe la Dunia mara tatu – 1958, 1962 na 1970, katika kipindi cha miaka 14 akicheza soka kimataifa ambapo alifunga jumla ya mabao 77 akiwajibikia taifa lake mara 92.


Fowadi matata wa Ureno Cristiano Ronaldo kupitia Instagram ametuma salama za pole si tu nchini Brazil na hasa kwa familia ya Pele, lakini pia kwa dunia nzima.


“Salamu zangu za pole zifike kote nchini Brazil na hasa kwa familia ya Edson Arantes do Nascimento. Kusema “kwaheri” pekee hakutoshi kuelezea hisia ambazo watu wako nazo kufuatia kifo cha Mfalme Pele. Pele atakumbukwa jana, leo na kesho kwa sababu aliibua kumbukumbu za kipekee akawa kipenzi kwa wapendao soka,” ameandika CR7 kama anavyofahamika raia huyo wa Ureno.


Naye mshambuliaji matata wa Paris Saint Germain (PSG) Kylian Mbappe amemuomboleza Pele akisema atakumbukwa milele.


“Mfalme wa kandanda hayuko nasi tena lakini mafanikio yake hayatasahaulika. Pumzika kwa amani,” ameandika Mbappe kwenye ukurasa wa akaunti yake ya Twitter.


Pele alizaliwa mjini Tres Coracoes nchini Brazil mnamo Oktoba 23, 1940.


Aliwahi kuuza njugu ili kusaidia familia yake kujikimu kimaisha.


Amekuwa akisumbuliwa na magonjwa ya figo na matatizo ya tezi dume.


Post a Comment

0 Comments