Ticker

6/recent/ticker-posts

Sadio Ntibanzokinza atua Simba Sc

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Klabu ya Simba imethibitisha kumnasa Sadio Ntibanzokinza na rasmi sasa atakuwa mchezaji wa klabu hiyo baada ya kutangazwa.


Simba imemtangaza kiungo huyo kupitia ukurasa wao wa Instagram. Simba SC imemsajili Saidi Ntibazonkiza kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu akitokea Geita Gold FC. Ntibanzokiza yupo jijini Mwanza kuungana na kikosi cha Simba kinachojiandaa na mchezo dhidi ya KMC.


Nyota huyo raia wa Burundi, aliwahi kuichezea Yanga na kuondoka kwenda Geita, uwezo wa kufunga, kutoa pasi za mabao umefanya Simba kuvutiwa na huduma yake.


Simba itaminyana na KMC katika mechi ya 18 ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Mchezo huo utahitimisha michezo yao mitatu ya Kanda ya Ziwa ambapo wameshinda mechi moja dhidi ya Geita Gold (5-0) kabla ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Kagera Sugar.Huo ni usajili wa kwanza kwa Simba katika dirisha dogo la usajili.


TETESI ZA USAJILI MPYA SIMBA SC NA ISHU YA NTIBAZONKIZA....….


Post a Comment

0 Comments