Ticker

6/recent/ticker-posts

Sababu za Barbara kujiuzulu Simba SC

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Barbara Gonzalez ameandika barua ya kujiuzulu wadhifa wake kama Afisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo kuanzia January mwakani.

“Nimetoa notisi ya mwezi mmoja ili nishiriki kuhakikisha kipindi kizuri cha mpito (transition) na makabidhiano (handover) na Menejiment mpya” “Ni jambo la fahari kwangu kwamba chini ya uongozi wangu, kwa kushirikiana na Rais wa Heshima wa Klabu, Mwenyekiti wa Klabu, Bodi ya Wakurugenzi, Wafanyakazi wenzangu, Wachezaji, benchi la ufundi, Wanachama, Washabiki,” ameandika Barbara

Barbara amesema amefikia uamuzi huo ili kutoa nafasi kwa Bodi mpya ya wakurugenzi itakayochaguliwa kwenye uchaguzi ujao kupata fursa ya kuchagua Mtendaji Mkuu na Menejimenti mpya itakayoendana a dira yao, pili kujipa nafasi ya kutimiza ndoto na fursa nyingine kwingineko.

“Kipekee nawashukuru wote tuliosafiri pamoja katika ndoto ya kuifanya Simba SC iwe kubwa kuliko ilivyokuwa huko nyuma, ni uamuzi mgumu sana kuacha kazi unayoipenda na uliyoifanya kwa moyo wote lakini ni ukweli pia kwamba mambo yote mazuri huwa na mwisho” amesema.

Post a Comment

0 Comments