Ticker

6/recent/ticker-posts

Nyota yako ya siku zijazo ni angavu sana kaka - Ozil amtia moyo Bukayo Saka

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Aliyekuwa kiungo wa Arsenal na mkali wa asisti Mezut Ozil ametuma ujumbe wa kutia moyo kwa kinda wa timu hiyo Muingereza Bukayo Saka baada ya Uingereza kubanduliwa nje ya mashindano ya kombe la dunia na mabingwa watetezi Ufaransa.

Ozil alimtaka Saka kutoyumbishwa na matokeo hayo na siku zote kuweka macho yake juu akitizama mbele kwani nyota ya mustakabi wake ni angavu mno kuliko hata jinsi anavyofikiria.

Pia mchezaji huyo alichambua kwa kiasi mechi hiyo na kusema kuwa Uingereza hawafai kutupiwa maneno kwa kupoteza dhidi ya Ufaransa kwani walijitahidi ila kwa bahati mbaya wakashindwa – lakini walishindwa na moja ya timu bora zaidi duniani – Ufaransa.

Aliwasifia kwa kudhibiti washambuliaji hatari wa Ufaransa wakiongozwa na nyota wa PSG, Kylian Mbappe na kusema kuwa kwa kumzuia tu kutowafunga, tayari walifanya kazi kuntu.

“Hamna haja ya kuona aibu Timu ya Uingereza. Utendaji mzuri dhidi ya Bingwa wa sasa wa Dunia, ukabaji mzuri dhidi ya Mbappe na wenzake, lakini Ufaransa ni mzuri sana kama kawaida. Mchezo mzuri kutoka kwa ndugu yangu Bukayo Saka - siku zijazo ni zako,” Ozil aliandika.

Katika mechi hiyo ya kufuzu nusu fainali ya kombe la dunia, kinda huyo wa Uingereza alikuwa nguzo bora katika kikosi cha kocha Gareth Southgate na alionesha mchezo wa kibabe dhidi ya Wafaransa mpaka kutuzwa kama mchezaji bora wa pambano hilo lakini juhudi zake hazikutosha kuisukuma Uingereza kwenye hatua ya nusu fainali.

Nahodha Harry Kane aliwakosesha Waingereza nafasi ya kupeleka mchezo huo katika majira ya ziada na pengine kwenye mikwaju ya Penalti alipoosa kufunga penalty ambapo walizawidiwa katika dakika za mwisho za mchezo na hivyo kufanay Ufarasna kushikilia ushindi wao wa mabao 2-1 hadi kipenga cha mwisho.

Post a Comment

0 Comments