Ticker

6/recent/ticker-posts

YAFAHAMU MAISHA YA PELE NJE YA UWANJA

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 


Maisha ya Pele nje ya uwanja yalikuwa yenye matukio mengi yenye rekodi sawia na taaluma yake.


Kando na kuwa mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea, Pele alioa mara tatu na kusaini kandarasi kadhaa za udhamini za matangazo zilizomvunia mamilioni ya pesa. 


Utajiri wa pele


Pele alivuna mamilioni ya pesa kutoka kwa matangazo ya Visa na Mastercard, na viatu vilivyotengenezwa kwa sehemu za tairi zilizosindikwa. 


Wakati wa Kombe la Dunia mwaka wa 1970, Pele alifikia makubaliano na Puma ambayo yangemletea $25,000(KSh3.0M) kwa mashindano hayo, pamoja na $100,000(KSh12.3M) kwa miaka minne iliyofuata na kupunguzwa kwa mauzo ya buti. 


Makubaliano hayo ambayo yalivunja mkataba kati ya Puma na wapinzani wake vikali Adidas kutomsajili Pele kwa sababu ya gharama zabuni, yalifanywa kwa masharti kwamba afunge kamba za viatu kabla ya mechi ya robo fainali ya Brazil na Peru kuanza. 


Alifanya ipasavyo huku kamera zikinasa wakati huo, na akajipatia dola milioni 2.85(3.5 Bilioni) katika kiwango cha pesa za sasa, bila kuhesabu alichopata kutokana na mauzo ya buti. 


Maisha ya pele na Familia yake


Licha ya kung'aa kwenye soka na kushinda mataji mengi, maisha ya Pele binafsi yalikuwa na matatizo chungu nzima. 


Mwanawe wa kwanza Edinho, ambaye alizaliwa miezi miwili baada ya ushindi wake katika Kombe la Dunia la 1970, alihukumiwa mwaka wa 2017 jela kwa zaidi ya miaka 12 kwa ulanguzi wa dawa za kulevya na utakatishaji fedha. 


Katika mahojiano mwaka huo na Bleacher Report, Edinho alifichua namna Pele alikuwa baba aliyetelekeza familia yake mara tu alipohamia New York kuchezea Cosmos na kumtema mkewe wa kwanza Rosemeri dos Reis Cholbi muda mfupi baada ya kuwasili Marekani. 


Baadaye alirudiana na Edinho, ambaye ni mlinda mlango wa zamani wa Santos, klabu ambayo ilimnoa Pele kama mchezaji wa soka. 


Hata hivyo, uhusiano wake na binti yake wa kwanza ulikuwa wa matatizo zaidi. Alikataa kumtambua Sandra Arantes do Nascimento kama bintiye, ambaye alizaliwa mwaka wa 1964 katika uhusiano wa kimapenzi na mjakazi wake. 


Hii ni licha ya mahakama za Brazil kuamua kuwa alikuwa mwanawe mwaka 1996 kufuatia mvutano na korti iliyodumu kwa miaka mitano. 


Sandra alifariki mwaka wa 2006 kwa saratani ya matiti akiwa na umri wa miaka 42.Pele alikataa kuhudhuria mazishi yake, na pia hakuwatambua wanawe wawili. 


Katika miaka yake ya mwisho ya 70, Pele alioa kwa mara ya tatu mnamo 2016, mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 42 Marcia Aoki. 


Pele na Aoki walikutana jijini New York katika miaka ya 1980 lakini walianza kuishi pamoja mwaka wa 2010. 


Pele na Muziki 


Pele pia alikolea kwenye tasnia ya muziki, baada ya kurekodi kutoa albamu kwa ushirikiano na mwimbaji na mtunzi maarufu wa Brazil Gilberto Gil. 


Muongo mmoja baadaye alitoa wimbo unaoitwa "Esperanca" ("Hope") ambao ulisherehekea Olimpiki ya 2016 jijini Rio de Janeiro. 


Alipokuwa akisherehekea kutimia umri wa miaka 80 mnamo 2020, Pele alirekodi wimbo na wachezaji wawili wa Mexico walioshinda Grammy, Rodrigo na Gabriela akisema ni zawadi yake. 


TANZIA: WANASOKA Watuma Salamu Za Pole Kufuatia Kifo Cha Pele



Post a Comment

0 Comments