Ticker

6/recent/ticker-posts

Liverpool Waizidi Ujanja Man Utd kwa cody gakpo

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

KLABU ya Liverpool imafanikiwa kukamilisha Usajili wa kiungo Cody Gakpo kutoka PSV Eindhoven, klabu yake ya PSV imethibitisha.

Cody Gakpo amekubali mkataba wa miaka sita na Liverpool, kama ilivyokuwa kwa Darwin Nunez msimu uliopita.


Miamba hao wa Uholanzi hawakuwa tayari kumuuza Gakpo mwezi Januari baada ya mchezaji huyo kuonyesha kiwango bora katika Kombe la Dunia akiwa na timu ya taifa ya Uholanzi huku United wakiwa na nia ya kumtaka tangu msimu wa majira ya joto. 


"PSV na Liverpool FC wamefikia makubaliano juu ya uhamisho wa Cody Gakpo," taarifa ya PSV ilisema.


"Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ataondoka mara moja kuelekea Uingereza ambako atapitia taratibu zinazohitajika kukamilisha uhamisho huo."


Ada kwajili ya uhamisho wa mchezaji huyo imefanywa siri, lakini mkurugenzi wa michezo wa PSV Marcel Brands amethibitisha kuwa ni mauzo ya rekodi kwa klabu.


Vyombo vingi vya habari vimethibitisha kwamba Liverpool walikuwa tayari kufikia bei ya pauni milioni 50 ambayo PSV ilitaka ili kumuuza Gakpo.


Baada ya kuonyesha kiwango bora katika fainali za Kombe la Dunia, kocha wa PSV Ruud van Nistelrooy alisema kuwa ni jambo lisiloepukika Gapko kuondoka katika klabu hiyo.


"Ingekuwa ni chaguo langu, basi napendelea angeondoka majira ya joto, lakini pia inaweza kuwa sasa," Van Nistelrooy aliiambia Voetbal International. "Unajua kuna wakati huwezi kukataa."


Post a Comment

0 Comments