Ticker

6/recent/ticker-posts

"Lionel Messi " adokeza kustaafu soka ya kimataifa baada ya fainali ya Kombe la Dunia

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi amedokeza kuwa mechi ya fainali ya Kombe la Dunia ambayo itachezwa siku ya Jumapili itakuwa mchezo wake wa mwisho wa kimataifa kushiriki.

Mshambulizi huyo nyota ambaye ana umri wa miaka 35 alidokeza kuhusu mpango wake wa kustaafu baada ya Argentina kufuzu kwa fainali ya Kombe la Dunia kufuatia ushindi dhidi ya Croatia Jumanne usiku.

"Nina furaha sana kwa kumaliza safari yangu ya Kombe la Dunia katika fainali, kucheza mchezo wa mwisho katika fainali. Hiyo kwa kweli inafurahisha sana," Messi aliwaambia waandishi wa habari baada ya mechi.

Messi alibainisha kuwa ameridhishwa na uchezaji wa timu yake na kusema furaha ya mashabiki wa Argentina vilimjaza raha moyoni. Alidokeza kuwa umri wa kucheza unampa kisogo na hivyo hawezi kuendelea zaidi.

"Kila kitu ambacho nimeshuhudia katika Kombe hili la Dunia kimekuwa cha kihisia, nikiona jinsi ilivyosherehekewa  Argentina. Kuna miaka mingi kutoka mwaka huu hadi kombe lijalo. Sidhani kama nitaweza kufanya hivyo. Kumaliza hivi ni vizuri, '' alisema.

Mshambulizi huyo matata alisisitiza kuwa Argentina itajitolea mhanga ili kushinda Kombe la Dunia baada ya kulipambania kwa miaka 36.

"Nimekuwa nikifurahia miaka michache iliyopita kuwa na timu ya kitaifa. Ninafurahia sana kila kitu kinachotokea kwetu. Kushinda Copa America, kucheza mechi 36 za Kombe la Dunia bila kufungwa, na kumaliza msururu wote huo kwenye fainali ni jambo la ajabu. Natumai watu nchini Ajentina watafurahia wenyewe na kile tunachofanya. Wasiwe na shaka kuwa tunajitolea kwa kila kitu kabisa,'' alisema.

Kufuatia ushindi wa Jumanne, Messi anasubiri mchuano wa Jumatano usiku kati ya Ufaransa na Morocco ili kujua watamenyana na timu gani kwenye fainali ya Kombe hilo ambayo itachezwa siku ya Jumapili.

Post a Comment

0 Comments