Ticker

6/recent/ticker-posts

KOMBE LA DUNIA LA FIFA QATAR 2022: Ufaransa yakata tiketi kucheza nusu fainali ya kombe la dunia

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Timu ya taifa ya Ufaransa imekuwa ya pili kukata  tiketi ya kucheza nusu fainali ya kombe la dunia baada ya kuifunga Uingereza bao 2-1 katika uwanja wa Al Thumama.

Iliwachukua Ufaransa dakika 17 tu kupata bao lao la Uongozi kupitia kwa mshambuliaji Aurelien Tchouameni

Na Uingereza waliendelea kupambana na  kipindi cha pili walifanikiwa kupata penati na Harry Kane alisawazisha katika dakika ya 54.

Ufaransa waliendelea na mashabulizi na kujipatia bao la pili katika dakika ya 78 mpira wa kichwa uliopigwa na Olivier Giroud ulikwenda moja kwa moja na kutinga wavuni kutokana na makosa yaliofanywa na Harry Maguire.

Uingereza itabidi wajilaumu wenyewe kwani walikosa penalti ambayo wangeweza kusawazisha baada ya Harry Kane kupiga juu mpira huo na kutoa mpira nje.

Kwa maana hiyo sasa ufaransa itakwaana na wawakilishi pekee wa Afrika Morocco katika nusu fainali ya pili Jumatano Desemba 14.

Post a Comment

0 Comments